30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TRA yaanza kuelimisha mfanyabiashara mmoja mmoja Kilimanjaro

Na Safina Sarwatt,Moshi

Mamkala ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza zoezi la kuwaelimisha wafanyabiashara mmoja mmoja mkoani Kilimanjaro lengo likiwa kulipa kodi kwa hiyari na kuongeza mapato ya Serikali.

Akizungumza na waandishi Habari Mjini Moshi Kaimu Meneja Elimu kwa mlipa kodi kutoka Makao Makuu, Rose Mahendeka amesema Elimu hiyo imeanza Dar es salaam na kwamba tayari karibia mikoa yote zoezi hilo limeshafanyika.

Amesema kuwa lengo kuu nikuongeza uwajibikaji na kuongeza ulipaji wa kodi ya Serikali kwa hiyari .

Mahendeka amesema kuwa elimu hiyo itatolewa kwa wafanyabiashara mmoja mmoja na kutoa taratibu za ulipaji kodi pamoja na kuwaelimisha kutunza kumbukumbu.

Amesema mzunguko wa fedha siyo mtaji hivyo wale ambao mauzo yao kwa siku ni 46500 wanatakiwa kutumia mashine ya EFDs kwani inasaidia kutunza kumbukumbu zao na kwamba watalipa kodi stahiki kulingana na biashara wanazofanya.

Mamkala ya Mapato Nchini TRA imeanza zoezi la kuwaelimisha wafanyabiashara mmoja mmoja mkoani Kilimanjaro lengo likiwa kulipa kodi kwa hiyari na kuongeza mapato ya Serikali.

Amesema kuwa lengo kuu nikuongeza uwajibikaji na kuongeza ulipaji wa kodi za Serikali kwa hiyari .

Mahendeka amesema kuwa elimu hiyo itatolewa kwa wafanyabiashara mmoja mmoja na kutoa taratibu za ulipaji kodi pamoja na kuwaelimisha kutunza kumbukumbu.

Amesema mzunguko wa fedha siyo mtaji hivyo wale ambao mauzo yao kwa siku ni 46500 wanatakiwa kutumia mashine ya EFDs kwani inasaidia kutunza kumbukumbu zao na kwamba watalipa kodi stahiki kulingana na biashara wanazozifanya.

Mahendeka amesema wapo wafanyabiashara wanatakiwa kutoa risiti ya vitabu na wale ambao wanatakiwa kutumia risiti za mashane za EFDs lakini baadhi hawafanyi hivyo kushindwa kupata kumbumbuku sahihi.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira amesema kumekuwa na malalamiko mengi kati ya mamlaka ya mapato Tanzania TRA na wafanyabiashara hivyo anaamini zoezi hilo litasaidia kutatua changamoto hizo.

Tilison Kabuje ambaye ni Meneja ni Msaidizi upande wa madeni Mkoa amesema Elimu hiyo itatolewa kwa wafanyabiashara wote katika wilaya sita za mkoa wa Kilimanjaro.

Kaimu Elimu kwa Mlipa kodi amesema Elimu hiyo inayotolewa ni pamoja na kusikiliza Changamoto za wafanyabiashara na kwenda kutatuliwa .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles