25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yazindua kadi ya biashara itakayosaidia Watalii

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

BENKI ya NMB imezindua kadi ya Biashara ambayo itawezesha Watalii kutohangaika wanapofanya manunuzi na malipo mbalimbali.

Uzinduzi huo uliofanyika jana katika Hoteli ya Neptune Pwani Mchangani Zanzibar, wakati wa mkutano wa mwaka wa Bodi ya Jumuiya ya Makampuni yanayotoa huduma ya Utalii Zanzibar (ZATO).

Akitoa ufafanunuzi wa matumizi ya kadi hiyo Afisa Mkuu wa Raslimali Watu NMB, Emmanuel Akonaay, amesema NMB imejipanga vyema kutoa suluhisho la huduma za kifedha, kwa kuwa na mifumo bora zaidi wa ubadilishaji fedha, pamoja na biashara ya kadi ambayo itawezesha watalii kutohangaika wanapofanya manunuzi na malipo mbalimbali.

Amefafanua kuwa kwa kufanya biashara, kadi hiyo inaweza kufanya miamala yote ikiwemo kulipia kodi na malipo ya serikali, ushuru, tozo za utalii, ukusanyaji mapato ya ndani, ada za TANAPA, Tamisemi, BRELA, Tanesco, TRA na ada ya paspoti ya kidijitali zote kupitia NMB mkononi.

‘’Benki ya NMB ipo  makini na uhitaji wa sekta ya utalii na wanaelewa wateja wanahitaji urahisi na ufanisi wa huduma za benki pamoja na suluhu mbalimbali endelevu za kibiashara’’alisema.

Amesema NMB imeweka kipaumbele kuhakikisha inasogeza huduma bora karibu na wateja, ili kuimarisha na kwenda na kasi ya Uchumi wa Buluu ambao kwa sasa ndio ngao ya Uchumi huo.

“Tuna huduma ya ubadilishaji wa fedha za kigeni (Forex) pamoja na Biashara ya kadi, pia tunalo jukwaa la biashara linalowezesha wafanyabiashara kufanya miamala kupitia tovuti zao (E-Commerce Platform), na tumewezesha matumizi ya kadi za malipo za ‘UnionPay,” amesema.

Pia amesema kadi hiyo  inakubalika katika kufanyia miamala kwenye mashine za kutolea fedha (ATM) na zile za kufanyia manunuzi (POS) za NMB, lengo likiwa kuleta huduma bora kwa wafanyabiashara kwenye setka ya utalii.

Hivyo benki hiyo kwa kushirikiana bega kwa bega na Jumuiya ya Makampuni yanayotoa huduma ya Utalii Zanzibar (ZATO) ilimeamua kuwarahishisha malipo na manunuzi ilikuleta manufaa, kwa kyumia  kadi mpya  ya malipo ya kabla (Prepaid Card) maalum kwa ajili ya wana ZATO.

Mapema akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Lela Muhamed Mussa, aliipongeza benki hiyo kwa kuzindua kadi hiyo, ambayo itarahisisha kufanya malipo ya aina mbali mbali pamoja na kuchangia pato la serikali kwa urahisi.

Amesema hivi sasa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kufanya malipo yoyote ya serikali kuwa ya njia ya kieletroniki, hivyo mfumo huo wa utasaidia kuchangia pato la nchi kwa utalii ili kukusanya fedha nyingi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Makampuni yanayotoa huduma ya Utalii Zanzibar (ZATO), Hassan Mzee, alipongeza benki ya NMB kwa kuwa nao pamoja katika kuhakikisha biashara ya utalii inapiga hatua kubwa.

Alisema kadi hiyo kwa kiasi kikubwa itawasaidia katika harakati zao za kukuza pato la utalii na sekta yenyewe, kwa ujumla na wana imani kuwa kupitia kadi hiyo watapata mafanikio makubwa.

Mwenyekiti huyo alifafanua kuwa hali ya utalii hivi sasa ni nzuri licha ya kuwepo kwa changamoto ya wimbi la nne la Uviko-19.

Alisema Zanzibar bado inaendelea kupokea idadi kubwa ya watalii jambo ambalo linadhihirisha kuwa serikali imeweka mipango mizuri ya kupambana na maradhi hayo.

Hata hivyo alisema jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na serikali kwa kuyafanyia kazi maagizo yote ya serikali ili kuhakikisha biashara ya utalii  inazidi kupiga hatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles