25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

NMB yapongeza ushirikiano wa Jeshi la Polisi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali imelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kusimamia usalama na ulinzi wa taifa jukumu ambalo Benki ya NMB imesema limechangia kwa kiasi kikubwa kuifanya taasisi hiyo kuwa kinara wa huduma za kifedha nchini.

Pongezi hizo zilitolewa juzi mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa maafisa waandamizi wa jeshi hilo ambako alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali wa maendeleo zikiwemo taasisi za fedha.

“Tunalipongeza jeshi letu la polisi kwa kuendelea kusimamia usalama na Amani nchini ambayo ni msingi mkubwa wa maendeleo wa mataifa yote duniani,” alisema Rais Samia kwenye hotuba yake ya kukifungua kikao kazi hicho kwenye Chuo Cha Polisi.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Rashid Masauni, amesema mchango wa NMB kulisaidia Jeshi la Polisi kuwahudumia watanzania ni wa kuigwa akitolea mfano wa benki hiyo kukubali kugharamia ununuzi wa samani za kituo chake kipya kitakachozinduliwa hivi karibuni huko Zanzibar.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi Ruth Zaipuna, aliuambia mkutano huo kuwa kutokana na Jeshi la Polisi kuwa chombo nyeti kinachosimamia ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao, benki hiyo itadumisha ushirikiano nalo na kulipa kipaumbele ili utendaji kazi wake uwendelee kuwa wa ufanisi na tija kwa taifa.

Moja ya maeneo muhimu kulifanikisha hilo, alifafanua, ni kulisaidia kukusanya mapato.

“Ushiriki wa NMB katika ukusanyaji mapato ya Serikali ni mkubwa sana. Makusanyo zaidi ya Sh trilioni 9.6 yalifanyika kati ya mwaka 2018 na 2021 ikiwa mwaka jana pekee tulikusanya Sh trilioni 3.7. Na kwa Jeshi la Polisi makusanyo kwa mwaka 2021 yalikuwa zaidi ya TZS bilioni 40,” alisema Zaipuna.

Aidha, aliwaeleza washiriki wa mkutano kuwa jeshi hilo lina mchango mkubwa katika mafanikio yao kama benki kiongozi wa huduma za kifedha nchini kwa kuiunga mkono kibiashara.

Huku akilipongeza jeshi la polisi kwa kuyalinda matawi yote 227 ya NMB yaliyo nchi nzima, alisema suluhisho walizonazo kwa ajili ya jeshi hilo ni pamoja na mikopo ya mishahara na nyumba, na huduma za bima na uwekezaji.

Akihitimisha wasilisho hilo, Zaipuna aliliomba Jeshi la Polisi kuendelea kushirikiana na benki hiyo kama mshirika mkubwa wa kifedha na kusaidia serikali kufanikisha ajenda ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.

Pia alibainisha kuwa NMB ina uzoefu na utaalamu wa kutosha kuweza kukidhi mahitaji ya chombo hicho kwenye upande wa suluhisho za kidijitali ambazo Rais Samia alisema ni muhimu kwenye mageuzi ya kuliboresha jeshi hilo.

“NMB inaongoza sokoni katika matumizi ya teknolojia kuwahudumia wateja ambapo zaidi ya asilimia 95 ya miamala yake inafanyika kidijitali nje ya matawi kupitia mawakala zaidi ya 10,000, ATMs zaidi ya 800 na huduma nyingine mbadala za kibenki kama NMB Mkononi na Internet Banking,” alisema Zaipuna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles