Niyonzima: Sitakuwa mtovu wa nidhamu tena

0
917

harunaaNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KIUNGO wa kimataifa wa timu ya Yanga, Haruna Niyonzima, amesema hataki tena kukumbwa na sifa ya utovu wa nidhamu katika timu hiyo, bali ataondoka katika klabu hiyo akiwa ameacha historia ya kiwango bora.

Niyonzima ambaye amerejea Yanga kuendeleza makali yake katika timu hiyo, hivi karibuni aliponea chupu chupu kutimuliwa kutokana na utovu wa nidhamu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Niyonzima alisema licha ya kuwa amebakisha mwaka mmoja kumaliza mkataba wake, amejiwekea malengo ya kuacha historia katika kikosi hicho.

“Sitaacha historia ya utovu wa nidhamu, nimejipanga kumaliza muda wangu kwa kuonyesha kiwango bora zaidi ya kile nilichokionyesha huko nyuma.

“Najua wengi watakuwa wananifikiria tofauti kutokana na mambo yale yaliyotokea hivi karibuni, lakini wasijali kila kitu kitabadilika,” alisema Niyonzima.

Mchezaji huyo alieleza kuwa anatambua mashabiki na wadau wa timu hiyo watakuwa wamekumbuka kiwango chake, hivyo wajiandae kumshuhudia tena.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here