24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Niyonzima rasmi Yanga

NA MSHAMU NGOJWIKE, DAR ES SALAAM

pg32 jan 23Sakata la Niyonzima kufukuzwa Yanga limechukua mwezi mmoja kabla ya wiki iliyopita kumalizana na kiungo huyo kuomba radhi ili aweze kurejeshwa kikosini.

Yanga ilitangaza kuvunja mkataba na Niyonzima kwa madai kwamba kwa kipindi kirefu mchezaji huyo amekuwa akifanya mambo na kuonyesha tabia ambazo si za kimichezo, gandamizi na ambazo zinaiathiri timu.
Ilidaiwa Niyonzima amekuwa akirudia mambo hayo, licha ya
klabu kumuonya mara kadhaa kwa barua na wakati mwingine kumkata mshahara, lakini tabia zake zimekuwa zikiigharimu timu.
Pia ilidaiwa alikuwa akichelewa na kukosekana mara kwa mara katika programu za timu, hususan anapokuwa amekwenda likizo au kutumikia timu yake ya Taifa ya Rwanda, ambako mara zote amekuwa akiondoka bila hata klabu kupata taarifa au kuombwa ruhusa.
Lakini pia Yanga imemtuhumu Niyonzima kushiriki katika mashindano ambayo siyo rasmi na bila kuruhusiwa na klabu, akiweka maslahi yake mbele na si yale ya klabu.
Kutokana na mambo hayo, Yanga ilidai Niyonzima ameshindwa kuishi kwa kufuata vipengele vya mkataba wake kwa kushindwa kuthamini kazi yake na utovu wa nidhamu kwa programu za Yanga, hususan mazoezi ya maandalizi.

Hivyo basi, Yanga ilimtaka mchezaji huyo kulipa dola za Kimarekani 71,175 (sawa na Sh milioni 143) kama gharama za kuvunja mkataba na kwamba itapinga usajili wake popote bila kulipwa fedha hizo.
Lakini wiki iliyopita mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara walimalizana na mchezaji huyo ambapo aliomba msamaha na kurejeshwa katika timu.

Akizungumza baada ya kurudi katika kikosi hicho, Niyonzima alisema anajisikia furaha kurejeshwa kwenye timu na atatumia uwezo wake kusogeza Yanga mbele zaidi.

“Nashukuru kwa nafasi hii nyingine, naipenda sana Yanga, nafurahi kuungana na wenzangu tena. Hata kama kipindi niliposimamishwa niliendelea kuwasiliana na wenzangu kuwatia moyo na kuwakumbusha kuwa msimu huu tubebe ubingwa, kwani hiyo ndiyo heshima yetu pekee na kudhihirisha ubora wetu.

“Yalisemwa mengi, eti nina mapenzi na Simba, hapana si kweli, sasa nimerudi mashabiki wa Yanga wasubiri vitu zaidi, ni kawaida kupishana, nina imani hayatatokea tena,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles