28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Nike watishia kuvunja mkataba wa Neymar

SAO PAULO, BRAZIL

KAMPUNI ya vifaa vya michezo duniani Nike, imetishia kujitoa udhamini wake kwa nyota wa soka wa timu ya taifa Brazil na klabu ya PSG kwa tuhuma za ubakaji.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, anakumbwa na kesi ya ubakaji ambapo juzi alifikishwa katika kitua cha polisi cha Sao Paulo nchini humo kwa ajili ya kujibu mashtaka baada ya mrembo Najila Trindade Mendes de Souza kuweka wazi kupitia SBT TV.

Neymar alidaiwa kufanya tukio hilo Mei 15, katika hoteli ya Sofitel, iliopo Paris nchini Ufaransa, lakini mwana soka huyo alikanusha vikali huku akidai ni mipango ya kutaka kumpoteza katika soka.

Nike ni moja kati ya kampuni ambazo zina mikataba na wachezaji wakubwa duniani, lakini siku zote inakuwa kampuni ya kwanza kuvunja mikataba kwa wachezaji kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji, tuhuma za kutumia dawa za kulevya na mambo mengine ambayo hayatakiwi kwa jamii.

Baada ya mrembo huyo kuthibitisha kuwa alibakwa na mchezaji huyo, Nike wameweka wazi kuwa wapo tayari kujiweka pembeni endapo kutakuwa na ukweli juu ya tuhuma hizo.

“Tumeguswa na tuhuma hizo na tupo karibu kufuatilia suala hilo hadi hatua za mwisho ili kuona ukweli uko wapi, kama kutakuwa na ukweli basi tutachukua maamuzi,” walisema Nike.

Kwa upande mwingine kampuni ya ndege nchini Brazil, Brazilian airline Gol Linhas Aereas Inteligentes SA, ambao ni wadhamini wa timu ya taifa ya Brazil ikiwa pamoja na Nike, wamedai kuwa wataendelea kuwa wadhamini wa timu hiyo hata kama Neymar atakutwa na kosa hilo.

“Tutaendelea kufanya kazi na timu ya taifa ya Brazil kwa kuwa ni timu na sio mchezaji binafsi, hivyo hatuwezi kukaa pembeni,” ilisema kampuni hiyo.

Brazil inatarajia kuwa mwenyeji katika michuano ya Kombe la Copa America ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 14, lakini mchezaji huyo hatokuwa kwenye kikosi cha taifa lake kutokana na kuwa majeruhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles