28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ni mwendo wa hesabu tu Taifa Stars kuonekana Cameroon mwakani

Na MAREGES NYAMAKA-DAR ES SALAAM

NENO kujifunza kutokana na makosa, lilionekana kufanya kazi katikati ya wiki iliyopita, baada ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars  kufanikiwa kulipa kisasi dhidi ya Cape Verde mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika(Afcon).

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Taifa Stars waliwatoa kimasomaso Watanzania kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Simon Msuva na Mbwana Samatta na kukiwezesha kikosi hicho kufufua matumaini ya kufuzu.

Ushindi huo ulikuwa na maana kubwa sana kwa kila Mtanzania baada ya siku chachu kufungwa mvua ya mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wao The Blue Sharks mchezo wa awali uliyochezwa Cape Verde.

Mchezo huo wa raundi ya tatu uliohudhuriwa na mashabiki wengi zaidi wakishangilia kuanzia dakika ya kwanza hadi kipyenga cha mwisho cha mwamuzi,  kikosi cha Taifa Stars na kilikuwa na mabadiliko ya wachezaji wawili pekee.

Mabaliko hayo alikuwa beki wa kati, Kelvin Yondani  aliyechukua nafasi ya David Mwantika mwingine akiwa mwanandinga mwenye kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani kiraka, Erasto Nyoni.

Mbali na ushindi uliyoleta tabasamu kwa asilimia kubwa ya Watanzania hasa waliohudhuria uwanjani hapo, wachezaji walicheza kwa kujituma na nidhamu ya hali ya juu wakitambua uzito wa kuvaa jezi ya nchi.

Hakukuwa na makosa mengi sana kama ilivyokuwa mchezo wa awali ugenini, hata katika mabadiliko yaliyofanya na kocha, Emmunuel Amunike yalikuwa na faida kubwa ya kuongeza nguvu na kuwapa presha zaidi wapinzani.

Feisal Salum Abdllah ‘Fei Toto’ aliyecheza kwa mara kwanza tangu timu iongozwe na Amunike  alionyesha ni kiungo aliyekamilika kucheza na timu ya aina timu yeyote, huku John Bocco akiwa mtulivu na mfno wa kuigwa.

Msimamo katika Kundi hilo L, Uganga wanaongoza na pointi zao 10, wakifuatiwa na Taifa Stars wenye alama tano,nyuma akiwapo Cape Verde alama nne, huku Cape Verde akiburuza mkia na pointi zake mbili.

Hadi hapo kwa taswira hiyo ni kucheza kimehesabu zaidi katika michezo miwili iliyosalia kwa kila mmoja,ingawa Uganda wanaoneakana kuwenye nafasi nzuri zaidi, kwani wanahitaji pointi moja pekee kufuzu.

Uganda akipata hata sare ya aina yeyote mchezo wa marudiano Novemba 16 mwaka huu, dhidi ya Cape Verde Uwanja wa nyumbani Mandela Namboole, utamfanya kufikisha alama 11, ambazo haziwezi kufikiwa na Cape Verde wala Lesotho.

Vita kubwa inaonekana kuwa kwa miamba wawili Cape Verde na Taifa Stars, kusaka nafasi hiyo ya kufuzu kwenda Cameroon mwakani kuwania mwali huyo anayoshikiliwa na mwandaaji wa michuano.

Taifa Stars atakuwa na kibarua cha kuwafuata kibonde, Lesotho hiyo hiyo Novemba 16 kusaka pointi tatu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kabla ya kurejea nyumbani kuwasuburi Uganda The Cranes hapo baadaye.

Kwa upande wa Cape Verde wao watakuwa na shughuli ngumu mbele ya Uganda wakiwa ugenini,ambao walifunga mchezo wa kwanza nyumbani na baadaye kumalizana na Lestoho.

Wawili hao kila mmoja anahitaji kushinda michezo yake,huku ikifika wakati wa kuombeana dua mbaya mpinzani apoteze kama ilivyo tamaduni la soka la Kiafrika, ingawa Stars akifanikiwa kushinda zote atakuwa tayari amefuzu.

Ni uwajibikaji unaopaswa kuendelea kuonyeshwa na Taifa Stars ukiambatana na nidhamu ya mchezo, kama ilivyoenekana mchezo uliyopita. Itakuwa ni faraja kwa kila Mtanzania akiwamo rais wa nchi,John Magufuli aliyetoa kitita cha milioni 50.

Hesabu kali inayotazamiwa zaidi huenda zikawabeba Uganda na Taifa Stars mchezo wa raundi ya nne kuwawezesha kufuzu hata kabla ya mchezo mchezo wa mwisho ni Uganda washinde mbele ya Cape Verde,huku Stars wakiwatungua Lesotho.

Matokeo hayo yatakuwa yanafanya msimamo kusomeka Uganda pointi 13,Taifa Stars alama nane, ambazo hazitafikiwa na Cape Verde wala Lesotho.

Licha ya kukosekana nahodha Mbwana Samatta mchezo ujao dhidi ya Lesotho kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano, bado Amunike ana kikosi kipana cha kusaka tiketi hiyo ya kufuzu.

Katika idara hiyo ya ushambuliaji anapohudumu Sammatta kuna John Bocco ambaye amaekuwa akitokea benchi ana kitu kikubwa mno cha kufanya ikichagizwa na uzoefu wake na soka la Afrika ikiwamo ngazi ya klabu akiwa na Azam.

Lakini pia Thomas Ulimwengu anayecheza ligi ya Sudan kwa sasa sambamba na akina Shaban Idd Chilunda, Farid Mussa wanaocheza ligi Daraja la Kwanza Hispania.

Jambo kubwa kuna muda wa kutosha kwa Amunike kuendelea kuzunguka viwanja mbalimbali vya Tanzania kushuhudia michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara huenda jicho lake likavuna dhahabu nyinyine ambayo ilikuwa haijapata nafasi.

Mfano mzuri ni Ibrahim Ajib kama kiwango chake kitaendelea kuimarika maradufu  hasa katika kutengeza mashumbulizi ikiwamo pasi zake za mwisho huenda akawa sehemu ya kikosi cha Stars kuongeza nguvu kuwazamisha Lesotho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles