26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Ney wa Mitego kutoka na Wizkid, Runtown

Nay-Wa-MitegoNA LETICIA BWIRE (TUDARCO)

MWANAHIP Hop, Ney wa Mitego, kwa mara ya kwanza amefanya wimbo wa ushirikiano na wasanii wa kimataifa kutoka nchini Nigeria, huku nyimbo hizo akipanga kuziachia mwishoni mwa mwaka huu.

Ney aliliambia MTANZANIA kwamba, wasanii alioshirikiana nao ni mkali wa wimbo wa ‘Ojogduma’, Wizkid na Runtown ambao wote ni kutoka nchini Nigeria.

“Wimbo nilioshirikiana na msanii, Runtown nitautoa mwishoni mwa mwaka huu, lakini nilioshirikiana na Wizkid nitauachia mwakani kutokana na nilivyopanga mambo yangu,” alifafanua Ney.

Hata hivyo, mwanahip hop huyo kwa sasa anatarajia kuachia wimbo alioupa jina la ‘Nyumbani kwetu’, ambao hajamshirikisha msanii yeyote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles