24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Ney wa Mitego kuachia nyimbo sita

nay-wa-mitegoNA THERESIA GASPER

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Elibariki Emanuel ‘Ney wa Mitego’, amefunguka kuwa mwaka huu anataka kuja kivingine tofauti na miaka ya nyuma.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ney wa Mitego alisema amekuwa akitoa nyimbo mbili au tatu kwa mwaka lakini katika mwaka huu anataka kuachia nyimbo sita.

“Nimekuwa nikitoa nyimbo mbili kwa mwaka au tatu, kwa sasa nataka nizidi kuwapa raha mashabiki wangu kwa mambo mazuri ambayo nimewaandalia mwaka huu, nitaachia nyimbo sita badala ya tatu kama watu walivyozoea,” alisema.

Alisema mwishoni mwa mwezi huu anatarajia kuachia video yake mpya  inayokwenda kwa jina la ‘Saka hela’ ambapo wimbo huo ukiwa na maadili mazuri kwa jamii na kuwaasa vijana wenzake wazidi kufanya kazi ili wawe na mafanikio.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles