28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA LIWALE

Na Mwandishi Wetu -Dar es Salaam


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale, Mkoa Lindi baada ya aliyekuwa Mbunge wake kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (Cuf), Zuberi Kuchauka, kujiuzulu na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kuchauka alijiuzulu hivi karibuni na kupoteza sifa ya kuwa mbunge hivyo kulifanya jimbo hilo kuwa wazi.

Akitangaza uchaguzi huo Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage, alisema tangazo la uchaguzi linakuja baada ya wao kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

“Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, ametutaarifu kuwepo kwa nafasi wazi ya ubunge katika Jimbo la Liwale mkoani Lindi, kuanzia Agosti 13, mwaka huu  kutokana na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Zuberi Kuchauka kujiuzulu uanachama wa Cuf na hivyo kupoteza sifa ya kuwa mbunge.

“Kwa mujibu wa vifungu vya 37 (1) (b), (5) na 46 (2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, tume inatoa taarifa kwa umma kuwa jimbo hilo lipo wazi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles