26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

NEC, CHADEMA JINO KWA JINO


Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM  |   

SASA ni jino kwa jino. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kuituhumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kabla Mkurugenzi wa tume hiyo, Ramadhan Kailima kujibu mapigo.

Kailima, jana alijibu tuhuma zilizotolewa na Chadema dhidi ya ya NEC kuwa itaendelea kuzingatia sheria, kanuni, maadili na taratibu mbalimbali wakati wa kuendesha chaguzi nchini.

Wakati NEC ikitoa msimamo huo, Chadema imepinga ikidai kuwa tume hiyo imepoteza weledi na haina uwezo wa kusimamia tena chaguzi

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kuhusu tuhuma ambazo NEC ilielekezewa na Mwenyekiti wa Chadema, kuwa haikutoa ushirikiano kwa chama hicho na ilikiuka sheria na taratibu za uchaguzi wakati  wa uchaguzi mdogo wa wabunge na madiwani uliofanyika Februari 17, Kailima alisema NEC haijibu malalamiko kwa kuzingatia  matakwa ya mtu bali matakwa ya katiba, sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi.

“Ni kwamba, shutuma na malalamiko yaliyotolewa na Mbowe yametusikitisha kwa sababu mbali na kumjibu kwa barua, tuliongea naye kwa njia ya simu.

“Haya madai kwamba tume haikuyajibu malalamiko yao siyo kweli, ni upotoshaji wa hali ya juu ambao haupaswi kufanywa na kiongozi kama yeye,” alisema Kailima.

Alisema kanuni, sheria, maelekezo na maadili ya uchaguzi yameweka utararatibu wa kushughulikia malalamiko na changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa uchaguzi, uteuzi na wakati wa kipindi cha kampeni ambapo malalamiko yote hushughulikiwa  na kamati za maadili zilizo maeneo ya uchaguzi kuanzia ngazi ya kata, jimbo na rufaa.

“Kwa masikitiko, Chadema walitekeleza hatua moja tu katika vipengele hivyo wakati wa uchaguzi, kipengele walichotekeleza ni pale baadhi ya …

Kwa habari zaidi ya jipatie nakala ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Ne Damu za Watanzania, hazitapotea bure. Kwenye NEC kuna viongozi wenye majukumu na elimu safi. Msijifiche nyuma za pazia. Mjiangalie kila mtu mwenye madaraka. Mtahukumiwa hapahapa duniani. Kifo cha binadamu moja tu ni doa. Kuna vifo vingi sana na damu zao zinalia. Nyinyi mnalipwa, mnafamilia, na mnafurahi. Damu za watu na ndugu zao si mchezo. Kama kuna nguvu zinawalinda, lakini nyinyi kama binadamu ambao mmakubali kutumika, hamuwezi kusafisha mikono yenu. Hakuna sabuni inayoweza kuitakatisha mikono ya kiongozi yeyote anayejihusisha kwa namna moja au nyingine kutoa maisha ya binadamu na ukafikiri yatakwisha. Ukubali kila unaponawa mkono wako, au mwili wako na sabuni, kuna damu nyingi na kelele za vifo vya watu wasio na hatia miilini na mioyoni mwenu. wengine mmeshindwa hata kutubu ingawa mmepewa nafasi ya kufanya hivi wakati huu wa Pasaka. Mtakwenda kumpokea Yesu hadharani mkiwa mmetapakaa na damu zisizo na hatia. Mtajificha mbele za ummati, lakini naamini roho zenu zinawasuta na hazina amani. Bwana aliyekupa wewe uhai ndiye aliyempa ndugu Aquilina, wasio na majina waliotelekezwa kwenye viroba, Waliofukiwa, pigwa bunduki na Mapanga. Mnayasikia mayowe yao mioyoni mwenu. Hata mnaposherekea, kunywa vijibia kucheka naamini hasa ndani kwenu kuna vilio na hakuna amani mioyoni mwenu. Mnaziona sura za watu na vilio vyao. Mungu awape nguvu mtubu, muombe radhi na mbadilishe mioyo yenu. Kumbukeni mna watototo, wake na ndugu,. Tubuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles