25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugai kuwaongoza wabunge Misri kuipa nguvu Stars

Na RAMADHAN HASSAN

-DODOMA

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai anatarajiwa kuwaongoza wabunge wa bunge hilo, kushuhudia fainali za mataifa ya Afrika (AFCON).

Mashindano hayo, yanatarajiwa kuanza June 21 mwaka huu nchini Misri,  ambapo Tanzania imepangwa kundi C,  pamoja na nchi za Kenya,Algeria na Senegal.

Akizungumza jana bungeni mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Spika Ndugai alisema amepanga kwenda kushuhudia fainali hizo.

 “Na wale wa awamu ya kwanza kama siku zile nne chache na mimi nitalipia nitaenda,  wale wa awamu ya kwanza tunaweza kuwa pamoja,”alisema Ndugai.

Akizungumzia utaratibu wa safari na gharama zake, Spika Ndugai alisema kutakuwa na awamu mbili za safari za kwenda  nchini Misri.

“Awamu ya kwanza ambayo itakuwa ya siku nne,  gharama zake ni Dola 720,  ikijumuisha tiketi za kwenda na kurudi, usafiri wa kwenda uwanjani na malazi.

“Mheshimiwa Ngeleja,  Mwenyekiti wa Bunge Sports  Club anawatangazia na kuwaombeni kwa ambao tunapenda kushuhudia fainali za mataifa ya Afrika nchini Misri mwaka huu.

“Tuendelee kujiandikisha kupitia Mheshimiwa Ngeleja, Ester Matiko, John Kadutu,Venance Mwamoto, Sixtus Mapunda na Cosato Chumi.

“Utaratibu mzima wa safari umeshatolewa kupitia mitandao yetu ya kibunge,  gharama za safari unachagua mwenyewe kama unataka kwenda awamu mbili ama moja.

“Lakini awamu ya kwanza ambayo ni siku nne ni dola 720 tu, usafiri na mambo mengine ukiwa Misri,  kupelekwa uwanjani na kurudi hotelini,”alisema.

Alisema awamu ya pili ambayo itakuwa ya siku sita,  gharama zake ni dola 770.

“Awamu ya pili ni ya siku sita,  hii gharama zake ni dola 770 tu kwa hiyo ukitaka kukaa siku zote ni sawa tu,”alisema.

Aliwaomba wabunge kwenda kuiunga mkono Stars ili wachezaji wajione wanadeni kwa Taifa.

“Tunaomba sana waheshimiwa wabunge tuunge mkono timu yetu,  ni miaka mingi hatujafika AFCON , wachezaji wakiwa wanacheza huku wanawaona wabunge wamekuja kuwaunga mkono naamini itawapa  nguvu kubwa zaidi,”alisema Ndugai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles