22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

NDIYO MACHINGA RUKSA POPOTE LAKINI KWA NIDHAMU

img_5753-1

JUZI Rais Dk. John Magufuli aliagiza wafanyabiashara ndogondogo, maarufu kwa machinga, wasibughudhiwe na wasiondolewe katika maeneo ya katikati ya miji wanayofanyia biashara kwani hakuna sheria inayowazuia.

Rais Dk. Magufuli alimwagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa kuwaondoa wafanyabiashara hao.

Rais akiwa na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan, alitoa agizo hilo juzi Ikulu na kuonya kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kulitekeleza aachie ngazi.

Kwamba maagizo yamekuwa yakitolewa mengi, mengine yanakuwa na mwelekeo wa kuchonganisha Serikali na wananchi.

Kwamba Rais Dk. Magufuli hapendi wamachinga wafanye biashara kwenye hifadhi ya barabara, lakini hakuna sheria katika nchi hii inayosema mtu wa biashara ndogondogo au machinga hatakiwi kufanya biashara katikati ya miji.

Kwamba wamachinga wasibughudhiwe kwa sababu hawakupenda kuwa machinga, na kumwagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja kuwaondoa machinga katika Jiji la Mwanza pamoja na mikoa mingine mpaka hapo mamlaka husika zitakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.

Kwamba Kigamboni hapa Dar es Salaam kulikuwa na wamachinga ambao wamehama vizuri kweli, wakatengenezewa miundombinu yao katika soko lao na sasa hivi wanafanya kazi vizuri, na viongozi wa machinga walishirikishwa.

Kwamba sasa Mwanza imekuwa ni amri tu, na wengine wanatumia hata msemo wa Hapa Kazi Tu ambao hausawiri hali halisi.

Kwamba pamekuwapo na maagizo mengi ambayo mengine yanakuwa na mwelekeo wa kuchonganisha wananchi na Serikali.

Kwamba suala linalomuudhi Rais ni kwamba alikwisha kuzungumza na makamu wake kwamba watatengeneza mazingira mazuri kwa watu hawa, watafutiwe maeneo ya kufanya biashara zao kwa utaratibu ulio mzuri.
Kwamba wajengewe mazingira ya kufanya biashara na wasizagae. Kwamba wakitaka kuwahamisha wazungumze nao kwa utaratibu mzuri na watakapopelekwa liwe ni eneo rafiki kwao na wafaidike kufanya biashara.

Tunaunga mkono mawazo ya Rais Dk. Magufuli na onyo lake kuwa amri yake isiwe chanzo cha wamachinga kufanya biashara na kujenga mabanda kila mahali.

Hii inahitaji nidhamu, wasizibe njia au ofisi au maduka ya wengine; na wanapofanya biashara wasijenge mabanda kwa sababu yanachafua mandhari ya miji.

Tunaunga mkono pia Rais Dk. Magufuli ya kuiagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha mara moja kuwaondoa wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Nyaligongo kilichopo katika Kata ya Mwakitolyo mkoani Shinyanga, na badala yake waachwe waendelee na shughuli zao, na leseni ya mwekezaji anayedai eneo hilo ni lake isitishwe.

Tunasema watu wengi wamejiajiri na mwekezaji ni mmoja tu.

Tunatoa hadhari kuwa maagizo ya Rais hayana maana kuwa wamachinga na wachimbaji wadogo waendeshe shughuli zao kwa kuvunja sheria.

Tunasema lazima wazingatie sheria, wasipange bidhaa zao ovyo mitaani na kuchafua mazingira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles