32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

NDEGE NDANI  YA HIFADHI SERENGETI ZAONGEZA WATALII

Na Mwandishi Wetu


IDADI ya watalii wanaokuja Tanzania imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka na kadiri Serikali kupitia Mamlaka zake mbalimbali  ikiboresha huduma na ufikaji wake eneo hilo muhimu kwa utalii wa Safari nchini.

Mchango mkubwa wa utalii katika uchumi wan chi unafahamika  na hivyo juhudi nyingi hufanywa kuwezesha ufanyaji shughuli katika maeneo mbalimbali na suala la usafiri wa haraka na wauhakika hutumika ili kufikisha watalii hususani katika mbuga ya Serengeti.

Hivi basi idadi ya watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), imeongezeka katika siku za hivi karibuni, kutokana na sekta hiyo kukua huku miundombinu ya barabara na viwanja vidogo vya ndege vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo vikifanyakazi vizuri.

Ofisa Utalii wa SENAPA, Evance Magomba, aliviambia vyombo vya habari mwishoni mwa mwaka jana kuwa, baada ya kujengwa jengo dogo kushugulikia wageni wanaowasili na wanaoondoka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera, idadi ya wageni imeongezeka huku wakala wa kampuni za ndege wakiweka wawakilishi wao katika uwanja huo. Hivi sasa kwenda na kutoka Serengeti kwa ndege  ya abiria  ya ratiba (scheduled) ni kitu cha kawaida na wengi wamefurahia utalii huo uliorahisishwa na usafiri wa anga.

Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa katika kipindi cha Januari hadi Septemba, mwaka jana, kumekuwa na safari za ndege 3,724, katika uwanja wa Seronera, huku uwanja wa Lobo, katika kipindi hicho kulikuwepo na safari 349 na uwanja wa Kogatende safari 564.

Kwenye Mfumo wa mbuga ya Serengeti  kwa maelezo ya Magomba  ni kuwa ndani ya hifadhi hiyo, kuna viwanja vidogo vya ndege saba, kikiwemo cha Seronera, ambacho ni kikubwa zaidi, chenye uwezo wa kupokea ndege kubwa yenye uwezo wa kubeba abiria 60, ikiwemo ya Shirika la Precision Air, inayofanya safari  za ratiba mara nne kwa wiki nahivyo mhitaji yoyote anaweza  kununua tiketi  mapema popote alipo ulimwenguni.

Kutokana na ukubwa wa hifadhi hiyo, ambayo ni eneo la kilomita za mraba 14,763 Serengeti  ni muhimu kwa utalii wa Tanzania kwani huingizia nchi fedha nyingi za kigeni na hivyo kuna  viwanja vingine vilivyosambaa maeneo mbalimbali ili kutoa huduma kwa urahisi na kuwawezesha watalii kupata muda mzuri wa kutembelea vivutio zaidi. Inapendeza vilevile kuwaona wanyama kutoka juu  kwenye ndege.

Viwanja  hivyo vingine kuwa ni Kogatenda, Lobo, Ndutu, Kirawira, Fort Ikoma na Lamai, ambavyo hutumika kwa malengo ya kurahisisha kufika eneo husika na kulingana na watalii wanavyopenda kuona vivutio maalumu.

Hifadhi ya Serengeti ni ya  siku nyingi nay a pili kwa ukubwa nyuma ya ile ya Mbuga ya Ruaha iliyopo mkoa wa Iringa.

Hifadhi hiyo ina wanyama wengi na wa kila namna na wale wanyama Muhimu Watano (Big Five) wa akina Simba, Chui, Tembo, Nyati na Faru.

Vilevile, alisema hifadhi hiyo ina uwezo wa kupokea wageni wa aina zote na kuna huduma za malazi, zikiwemo hoteli saba za kifahari na kambi za kudumu sita na hivyo kuifanya mbuga hiyo kuwa moja ya maajabu saba ya Afrika kutokana na uwepo wa Mhamo wa Wanyama (Great Migration) kutoka mbuga hiyo kwenda Masai Mara kila mwaka amabakao wanya ma zaidi ya milioni moja huhusika kwenye msafara huo.

Alisema huduma za kitalii nchini zimeongezeka kwa kasi baada ya serikali kupitia Bodi ya Utalii (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wadau wengine wa utalii, kutangaza kwa kiwango kikubwa sekta ya utalii.

Vilevile kuna kampeni kubwa inafanyika ya utalii wa ndani  na unafanikiwa.

“Kipekee tunawakaribisha wananchi kutembelea hifadhi zetu kwa sababu zipo bei maalumu kwa ajili yao,” alisema Magomba.

Kutokana na mahitaji makubwa ya huduma na ufinyu wa wa hali ya jingo alishauri TANAPA kuongeza ukubwa wa jengo la abiria wanaowasili na kuondoka na huduma zingine muhimu ili kuwawezesha watumiaji wa jengo hilo kupata huduma za kiwango cha juu, hasa wakati wa msimu wa utalii.

Serengeti na Ngorongoro ndio mbuga zinazoingiza mapato makubwa kwa TANAPA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles