29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ndayiragije: Kenya watapigwa tu

ONESMO KAPINGA, NAIROBI KENYA

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),  inatarajia kushuka uwanjani leo kucheza na Kenya(Harambee Stars), katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi ya Ndani (Chan), utakaochezwa kwenye Uwanja wa Karasani, jijini hapa.

Mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, timu hizo zilitoka suluhu, hivyo Taifa Stars inahitaji ushindi ili iweze kujihakikishia kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Stars, Etienne Ndayiragije, alisema wamekuja Nairobi kutafuta ushindi, baada ya timu yake kupata matokeo ya sare na watapambana kwa hali yoyote kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

Ndayiragije alisema, anatarajia kutumia mbinu mpya hasa baada ya kusoma udhaifu wa wapinzani wao Harambee Stars katika michezo wa kwanza uliomalizika kwa matokeo ya kutofungana.

Aliwataka Watanzania wasiwe na wasiwasi, kwani ana uhakika timu yao itasonga mbele katika michuano hiyo, baada ya kumaliza dakika 90 ya mchezo wa leo dhidi ya Harambee Stars.

Kocha huyo, alisema amefanya marekebisho ya kiufundi na mbinu katika kikosi hicho  ili kuhakikisha Harambee Stars, hawapati nafasi ya kupata ushindi, ingawa alikiri wazo kuwa utakuwa ni mgumu kwa kuwa kila timu itahitaji ushindi.

Kwa upande wake, Nahodha wa Taifa Stars, John Bocco, amesema wamejiandaa vizuri na anaamini ushindi utapatikana katika mchezo wa leo, licha ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa matokeo ya suluhu.

Bocco alisema watapambana kufa au kupona kusaka ushindi dhidi ya wenyeji wao Harambee, ili waweze kutinga hatua inayofuata ya michuano hiyo.

“Tumekuja hapa kwa lengo moja ya kutafuta ushindi utakaotuvusha hatua inayofuata, tunajua mchezo utakuwa mgumu, lakini tumejiandaa na tutapambana,” alisema Bocco.

Nahodha huyo, alisema anaamini marekebisho yaliyofanywa na kocha wao Ndayiragije yatawawezesha kutimiza malengo yao ndani ya dakika 90 za mchezo huo.

Katika hatua, nyingine, Balozi ya Tanzania nchini Kenya, Pindi Chana alisema atakuwapo uwanjani kwa lengo la kuungana na Watanzania wengine wanaoishi jijini hapa, kuhamasisha ushindi kwa Taifa Stars.

Pindi alisema ataongoza mwenyewe msafara wa wachezaji wa Taifa Stars kuelekea uwanjani, ili wasikutane na vikwanzo vyovyote njiani ambavyo vitaweza kuwatoa mchezoni.

 Alisema kutokana na maandalizi yaliyofanywa na benchi na ufundi la Stars, anaamini        ushindi utakuwapo na Tanzania kusonga mbele katika michuano hiyo.

Bolozi Pindi alisema anakiamini kikosi cha Stars, hivyo hana shaka kabisa dhidi yao.

Alisema pamoja na hali ya hewa ya Nairobi kuwa ni ya baridi kali, lakini itakuwa ni nzuri kwa Taifa Stars kupambana na kuweza kuondoka na ushindi ambao wanausubiri kwa hamu na Watanzania wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles