KULWA MZEE, DAR ES SALAAM
Nchi za Afrika zimetajwa wakati wa kumbukizi ya kifo cha Imam Ayatollah Khomeini kwamba ni mfano kwa jinsi zilivyopambana na janga la corona kwa mtazamo wao.
Shekhe Musabaha Shabani ametolea mfano nchi hizo katika mjadala kwa njia ya mtandao kuhusu kumbukizi ya kifo cha Imam Ayatollah Khomeini iliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Kiislamu cha Ubalozi wa Iran Dar es Salaam
” Imam Khomeini aliitazama dhuruma katika nyanja zote, si mtu kunyimwa haki tu, bali hata kuingiziwa fikra ambazo mtu fulani anataka, kila nchi inapaswa kuwa na haki ya kujiamulia mambo yake, mfano nchi za Afrika jinsi zilivyopambana na corona kwa mtazamo wao,” alisema.
Akimzungumzia Imam Khomeini alisema katika nyanja ya haki, uchumi na kisiasa ni miongoni mwa mambo yaliyokemewa na Imam huyo.
Alisema kiongozi huyo aliitazama dhuruma katika nyanja zote ikiwemo kunyimwa haki na hata kuingizwa fikra za mtu mwingine.
“Imam Khomeini aliitazama dhuruma katika nyanja zote, si mtu kunyimwa haki tu, bali hata kuingiziwa fikra ambazo mtu fulani anataka, mfano nchi za Afrika jinsi zilivyopambana na corona kwa mtazamo wao, lazima watu wote, nchi zetu ziwe na haki ya kujiamulia mambo yake,” alisema Msabaha.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Avazeli Lwaitama amesisitiza kwamba binadamu wa mataifa mbalimbali wanaweza kuchangia dhana ya demokrasia nchini mwao
“Mimi sio muislamu namzungumzia Imam Khomeini kwa matendo yaka yenye faida kwa binadamu wote.
“Imam alikulia katika nchi mbalimbali na mazingira mbalimbali, hali hiyo ilimfanya awe na upeo mpana uliozama katika utamaduni wa Kiislamu kuhusu ukombozi wa binadamu,”alisema Dk Lwaitama.
DK. Lwaitama alisema Imam alikuwa akisema kwamba binadamu hakuzaliwa kufanya mzaha, amezaliwa kwa malengo ya kwenda mbali ikiwemo kuchangia kuwepo kwa demokrasia kama Imam katika uhai wake nchini Iran.