25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

NBC yaja na Wajibika

Anthony Mavunde
Anthony Mavunde

Na Ruth Mnkeni, Dar es Salaam

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imekuja na mfumo wa ‘Wajibika’ wenye lengo la kuwaandaa vijana wahitimu wa vyuo na taasisi za elimu ya juu kuingia katika soko la ajira.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwishoni mwa wiki, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde, alisema changamoto hiyo inachangiwa na idadi kubwa ya wahitimu kutoendana na uwezo wa kuajiriwa sekta iliyo rasmi.

Alisema ongezeko la vijana linalokadiriwa kuwa milioni 16.2 kwa sensa ya mwaka 2012, limechangia baadhi ya vijana kukaa bila kazi, hivyo kushawishika kirahisi kujiunga na makundi yasiyofaa kama ‘panya road’ ugaidi, ujambazi, ujangili na biashara haramu ya dawa za kulevya na ngono.

“Kipekee napenda kuipongeza NBC kwa kubuni na kuanzisha programu hii ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa sera, mikakati na mipango ya Taifa ya kupambana na changamoto zinazowakabili wananchi wake ikiwamo ya ukosefu wa ajira,” alisema Mavunde.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Mkurugenzi wa bodi hiyo, Dk. Kassim Hussein, alisema mpango wa ‘Wajibika’ unalenga kutatua changamoto inayotatiza jamii ambayo ni uwezo wa kuajiriwa au kujiajiri.

Alisema ‘Wajibika’, tayari imetambulishwa kwa  vyuo 25 Dar es Salaam na kupata baraka za Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles