25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Nawapongeza Wamasai waliokubali kuhama Ngorongoro

Na Eston Mujumba

Ndugu Mhariri kwanza nachukua fursa hii kuipongeza Serikali yetu sikivu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo mazuri inayofanya.

Ni wazi kwamba mambo mengi yameendelea kufanyika ambayo kama wananchi tunapaswa kujivunia ndani ya nchi yetu.

Nikijielekeza kwenye mada yangu ndugu mhariri napenda niwapongeze ndugu zetu Wamasai ambao wameamua kuunga mkono uamuzi mzuri wa Serikali wa kuwahamisha kutoka hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha kwenda Msomela mkoani Tanga.

Ni jambo la kuwapongeza wamasai walio amua kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao kwasababu Ngorongoro hapakuwa sehemu rafiki kwa ustawi wa hifadhi ile.

Kukubali kuhamia Msomela ni wazi kuwa itakuwa na faida hata kwa vizazi vyao kwani tayari wamejengewa makazi ya kudumu na Serikali.

Hata Wajukuu na Vitukuu watakuwa na sehemu ya kurithi ikiwamo mashamba na sehemu ya kuchungia mifugo yao tofauti na ilivyokuwa awali kuendelea kukaa ndani ya hifadhi ya Ngorongoro bila kuwa na makazi bora na ya kudumu achilia mbali eneo la malisho.

Kwa sasa wananchi hawa wanafurahia kuishi kwenye nyumba bora zenye umeme, maji na pia wana uwezo wa kuendeleza chochote tofauti na ilivyokuwa awali ambapo sheria za hifadhi ziliwa haziruhusu.

Hivyo, kwanza nihitimishe kwa kuipongeza Serikali ya Rais Samia kwa uamuzi huo, pili niwapongeze Watanzania wenzetu waliokubali kuhama huku nikiendelea kuwasihi waliobaki pia kuhamasika kuhamia Msomela.

Mwandishi wa barua hii ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Chuo Kikuu Cha Tumaini Dar es Salaam(TUDARCo).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles