27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Nani yupo nyuma ya Burundi?

Na ELIYA MBOBEA
-ARUSHA


HAKUNA lugha inayoweza kutumiwa kufafanua “dharau” iliyoonyeshwa na nchi ya Burundi kwa wanachama wenzake watano wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Kilichofanywa na Burundi au Serikali ya Rais Pierre Nkurunziza, kinaweza kufanywa pekee na mataifa yenye jeuri ya kiuchumi na nguvu za kijeshi na si Burundi.

Mkutano Mkuu wa 20 wa mwaka au (Summit), ya Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC), unaotambulika kikatiba kwamba lazima ufanyike kwa mwaka, haukufanyika mjini Arusha.

Sababu kuu za kutofanyika mkutano huo kwa marais waliofika waliohofia kuvunja Katiba ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo kutokana na kuwataka wawepo wote kwenye mkutano mkuu huo.

Yapo mengi yaliyojificha nyuma ya “kiburi” cha Burundi kuacha kuhudhuria mkutano, na hata kushindwa kutuma mwakilishi wala kutoa taarifa kama walivyofanya Rais wa Rwanda Paul Kagame na Sudani Kusini Salva Kiir, walituma wawakilishi.

Binafsi viongozi waliotuma wawakilishi walitambua umuhimu wa mkutano huo, lakini pia kuwapa heshima viongozi wenzao watakaohudhuria.

Yapo yaliyopangwa kufanywa na viongozi hao kwa afya na uhai wa Jumuiya lakini hayakuweza kufanikiwa kutokana na mwanachama mmoja kutofika. Hii ni hasara kubwa sana na doa kwa uhai wa Jumuiya hiyo kwani kuna baadhi ya makubaliano mbalimbali kwa manufaa ya EAC yalipaswa kupitishwa.

Ili shughuli hizo zifanikiwa ililazimu kutumika gharama kubwa ya fedha ambazo ni kodi za wananchi wa EAC na michango ya wafadhili kutoka nje ya Jumuiya.

Sasa haya yote hayakuonekana kwa Burundi wala kujitafakari ikatuma mwakilishi atakayewezesha angalau basi kuruhusu mkutano ufanyike ili kuepuka kupoteza fedha nyingi.

Wapo kina mama na wafanyabiashara kutoka nchi wanachama waliofika kuuza bidhaa zao kwenye mkutano huo ambao takribani kila nchi ilikuwa na watu zaidi takribani 40.

Hawa wote na wengine, walisafiri kutoka makwao kwenda Arusha kufanya biashara kama ambavyo nchi hizo zinahamasisha ushirikiano wa pamoja katika biashara na kutembea.

Ukiondoa wafanyabiashara kwenye mkutano huo walikuwapo pia wawakilishi kutoka nchi wafadhili za Ulaya.

Nchi wafadhili hadi sasa ndio zinatajwa kuchangia fedha nyingi za maendeleo, utawala katika jumuiya hiyo, kutokana na baadhi ya nchi wanachama ikiwamo Burundi kutotoa michango yao kwa wakati.

Katika mazingira hayo ya uchelewesheji michango kwa nchi wanachama, bado anakuwapo kiongozi mkuu wa serikali ambaye hahangaiki kutoa taarifa kwa viongozi wenzake ili kuepuka gharama.

Jeuri hii ambayo hata Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk.Augustine Mahiga alionyesha kushangazwa na kitendo hicho.

Mahiga katika mazungumzo yake na wanahabari alikiri jambo hilo halijawahi kutokea kwa Rais kushindwa kuhudhuria mkutano mkuu, lakini pia kushindwa kutoa kabisa taarifa wala mwakilishi.

Yapo mengi ya kujiuliza nani yupo nyuma ya ukimya huo wa Serikali ya Burundi mpaka iwadharau wanachama waasisi wa Jumuiya hiyo?

 

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles