NAIROBI, KENYA
MKALI wa muziki nchini Kenya, David Mathenge ‘Nameless’, amefunguka kwa mara ya kwanza tangu atoke hospitalini baada ya kulazwa kwa wiki tatu, hivyo msanii huyo amedai alikaribia kupoteza maisha.
Ni wiki sasa tangu Nameless atoke hospitalini, sasa amesema yupo tayari kurudi katika kazi yake ya muziki kutokana na afya yake kuwa sawa.
“Sikuwa na imani kama ningeweza kurudi katika hali yangu ya kawaida, lakini ninashukuru sasa nina nguvu na nipo tayari kurudi jukwaani na kuwapa burudani mashabiki wangu.
“Ukweli ni kwamba nilikuwa kwenye wakati mgumu kwa kipindi chote ambacho nilikuwa hospitalini, kuna wakati nilikuwa nawaza kifo, lakini ninamshukuru Mungu kwa kunirudisha kwenye hali yangu ya kawaida japokuwa si kwa asilimia 100,” alisema Nameless.