25.4 C
Dar es Salaam
Thursday, January 9, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Naibu Waziri atoa onyo kwa wanafunzi Z’bar

Na Khamis Sharif-ZANAIBAR

NAIBU Waziri wa  Wizara  ya Kazi, Uwezeshaji,  Wazee ,Wanawake na Watoto, Shadya Mohamed Suleiman amewataka wanafunzi wa Jimbo la Magomeni kushughulikia masomo yao na kujiepusha na mambo ya tamaa kwani  yanaweza kuwapelekea kutofikia malengo yao.

Hayo aliyasema hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika utaoji wa zawadi katika shule za Jimbo la Magomeni wakati wa sherehe ya utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofaulu kuingia michepuo , kidato cha pili na kidato cha tano kwa mwaka 2017/2018.

Alisema ili wafanikiwe zaidi katika elimu ni lazima wawe wasikivu na wavumilivu kwa kufuata ushauri wa walimu ndipo watafanikiwa kwani elimu ndio mustakabali mzima wa maisha  na kuwataka waongeze bidii katika masomo  kwani wao ndio wataalamu  watarajiwa wa hapo baadae.

“Acheni tamaa za kutamani vitu ambavyo wazazi hawana uwezo navyo mambo haya ndio yanayoweza kukuharibieni malengo yenu mliojiwekea ya baadae shuhulikieni masomo yenu,” alisema Shadya.

Pamoja na hali hiyo aliwapongeza watoto wa kike kwa kufaulu wengi na kuwataka waache ukimya pale wanapokabiliwa na vitendo vya udhalilishaji kwa kuwaripotia wazee wao ili sheria zichukuliwe kwa haraka.

Aliwataka walimu kuongeza bidii  kwa kuwa karibu na wanafunzi ili kuwashajihisha na serikali inawaandalia walimu mazingira mazuri na kuwaondolea changamoto zinazowakabili.

 “Vitendo vya udhalilishaji vipo hivyo wazazi wenzangu tujitahidi kuwa na watoto wetu kila wakati ili kuzijua nyedo zao za kila siku, na ukimuona ana kitu cha thamani tusiogope kuwauliza na kufatilia wapi kapata,” alisema Shadya.

Nae Mbunge  wa Jimbo la Magomeni, Jamal Kassim na Mwakilishi Rashid Shamsi Makame, walisema wameanza kutoa zawadi hizo tangu walipoanza kuingia madarakani.

Wakitoa wito kwa wazee na walimu kuwa na mashirikiano kwa lengo la kuona vijana hao wanafikia nafasi nzuri kielimu kwani duniani kote sasa elimu ndio inaleta maendeleo na mafanikio hayawezi kupatikana iwapo watakosekana wasomi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles