24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Naibu Waziri aipa TBC wiki moja


Na Anitha Jonas-WHUSM, Namanga

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ameuagiza uongozi wa Shirika la Utangazaji  la Taifa (TBC) Kanda ya Kaskazini kukamilisha ujenzi wa kituo cha kurusha matangazo kinachojenga Makao Makuu ya Wilaya ya Longido ndani ya wiki moja.

Agizo hilo alilitoa jana wilayani Longido alipotembelea kituo cha kurusha matangazo ya TBC kinachojengwa wilayani hapo kwa lengo la kutatua kero ya kukosekana kwa usikivu wa matangazo ya TBC ambapo wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakisikiliza radio za nchi jirani na hiyo  imewafanya kukosa taarifa zenye ukweli na uhakika za ndani ya nchi.

“Chumba hikii cha kuhifadhi busta na mitambo mingine ni kidogo sana na ujenzi wake siyo wa kuchukua muda mrefu hakikisheni mpaka Januari 10, muwe mmekamilisha ujenzi wa kituo hichi wananchi wa Longido wanakiu kubwa ya kutaka kusikia matangazo kutoka  chombo hiki cha serikali chenye habari za ukweli na uhakika na hii ni haki yao,” alisema Shonza.

Pamoja na hali hiyo pia aliwasisitiza viongozi hao wa TBC kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho cha kurushia matangazo kinajengwa kwa kutumia vifaa imara kwani serikali ilitenga bajeti yenye fedha za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha usikivu unaboreshwa katika maeneo ya  mipakani  na malengo ya serikali ni kabla ya mwa 2020 kero hii ya usikivu iwe imekwisha.

Kwa Upande wa Katibu Tawala Wilaya ya Longido, Toba Nguvila asisitiza kuwa ukosekanaji wa usikivu wa matangazo ya TBC wilayani hapo umekuwa ni changamoto kubwa  kwa utoaji na upokeaji  wa taarifa  muhimu kuhusu shughuli za kiserikali kwani  wakazi wa eneo hilo wanashindwa kupata taarifa hizo kwa wakati ukizingatia jamii ya wakazi hao ni wafugaji na huishi kwa kuhama hama.

“Tungependa matangazo ya TBC yaanze kusikika hapa Longido haraka kwani yapo mambo mengi yanayohitajika kutolea elimu kwa wakazi wa eneo hili kupitia vipindi vya redio ,kwani TBC ni chombo kinacho rusha habari zenye ukweli na uhakika hivyo tungependa  wananchi wa hapa nao waweze kusikia matangazo yenu,” alisema Nguvila.

Naye Meneja wa TBC Kanda ya Kaskazini, Gerald Uisso alieleza kuwa ameyapokea maelekezo hayo na atahakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya muda na vifaa vyake kuwa veye ubora.

Meneja huyo aliwahakikishia viongozi hao mara baada ya kukamilika ufungwaji  wa mitambo hiyo  usikivu wa matangazo katika eneo hilo utakuwa uko imara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles