32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Naibu Meya atoa siku tano kufanyika kwa uchaguzi

RAYMOND MINJA, IRINGA

Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa,Joseph Lyata, ametoa siku Tano kwa kikundi cha wafanyabiashara wa minadani (WAMMA) kuitisha uchaguzi na wa viongozi wapya ili kuepusha migogoro isiyokuwa na lazima.

Uamuzi huo wa Naibu Meya umekuja mara baada ya viongozi wa kikundi hicho kijiuzulu nafasi zao jana Mei 24 .

Akizungumza na wanachama hao leo Mei 25, kwenye mkutano aliouitisha amesema mara baada ya kusikiliza pande zote mbili viongozi na wanachama ni vema kufanya  uchaguzi wa viongozi wapya ili kuendesha kikundi hicho.

“Ndugu zangu sasa tumefikia sehemu nzuri tumefanya mazungumzo kwa
amani bila hata ya kuwepo kwa polisi na viongozi wamekiri mapungufu
yao na katika hali ya kawaida hakuna binadamu asiyekuwa na mapungufu
na hata nyie wanachama mna mapungufu yenu hivyo basi ndani ya siku
tano tumekubaliana hapa tuitishe mkutano mkuu na tufanye uchaguzi wa
viongozi wetu maana hawa waliopo hawapo kisheria “ amesema lyata

Amesema wafanyabiashara wadogo wadogo ni watu muhimu sana kwenye nchi hii na ndiyo maana Rais Magufuli amekuwa akiwatetea na kuwapigania wafanyabiashara wadogo hasa machinga  na ndiyo maana akatoa maelekezo kwa viongozi aliowateuwa kuwapigania
wafanyabiashara hao ili wasibughudhiwe na mtu yoyote .

“Ndugu zangu nyie ni watu muhimu sana mmekuwa mkifanya kazi nzuri na
ndiyo maana nchi yetu inasonga mbele  kwani sote tunategemeana na ndiyo
maana leo tumekuja hapa pamoja na watendaji wa manispaa ili kufanya
kikundi hiki kisife bali kiendelea na baadae hata kuja kuwa benki kama
vikundi vingine vilivyoanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles