25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

NACOPHA yaishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa dawa za ARVs

Na Faraja Masinde, Mbeya

BARAZA la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini (NACOPHA), wameishukuru Serikali kuendelea kutoa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi bure na kwamba hatua hiyo imesaidia kuimarisha afya zao.

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Leticia Mouris alitoa kauli hiyo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kitaifa yalifanyika jijini Mbeya.

Waziri Mkuu Kasiim Majaliwa(Kushoto) akiwa sambamba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Jenista Mhagama baada ya kutembelea mabanda mbalimbali yaliyokuwa kwenye viwanja vya Ruanda nzovwe, Mbeya.

Alisema Serikali imewasaidia Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVVU) kusambaza dawa kwenye vituo mbalimbali vya Afya na kusaidia watu hao kupata dawa hizo kwa uhakika.

Alisema Baraza linaunga mkono mkakati wa Serikali katika kufikia 95 tatu ambazo zinalenga kutokomeza maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi kwa kuwakinga wengine na kuhakikisha waendelea kuimarisha umoja na utengamano kupitia majukwaa yao.

Alisema katika kuhakikisha baraza hilo linafanyaka kazi kwa ufanisi wameanzisha mabaraza 180 yakihusisha wanawake na vijana na kwamba jumla WAVVU 600000 wamejiunga kwenye baraza hilo.

Mouris aliwahamasisha wananchi kuendelea kupima afya zao na kuishi kwa malengo ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Aidha alisema Baraza hilo linakabiliwa na tatizo la unyanyapaa, Ukatili wa Kijinsia kwani linachangia kasi ya maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi.

Aliongeza kamati za kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi kuanzia ngazi za Vijiji hadi Wilaya zimesaidia kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera alisema kuwa wiki ya maadhimisho ya Ukimwi mkoani humo yamekuwa na mafaniko makubwa ikiwamo wajasirimali kuiongezea kipato.

Mafanikio mengine ni kuwezesha jumla ya wanawake 146 waliofanyiwa uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa kizazi na pia jumla ya wananchi 1,172wamejitokeza kupima maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi ambapo kati yao waliokutwa na maambukizi I29 sawa na asilimia 2.5.

“Sambamba na hayo kumekuwa na mwitiko mkubwa kwenye uchanjaji wa chanzo ya Uviko-19, ambapo wengi wamejitokeza kupata chanjo hiyo muhimu kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo, hivyo kama mkoa tunashukuru sana kwa heshima hii tuliyopewa na kama itawapendeza waratibu tupewe tena fursa hii mwakani,” alisema Homera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles