24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Mzindakaya ajitumbua NDC

Crisant Mzindakaya
Crisant Mzindakaya

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Crisant Mzindakaya, amejiondoa katika wadhifa wake kwa kile kilichoelezwa kuomba kupumzika.

Amechukua hatua hiyo ikiwa ni miezi michache tangu Rais Dk. John Magufuli aanze kuifanyia kazi ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo NDC nayo inaguswa.

Taarifa kutoka ndani ya NDC ziliimbia MTANZANIA jana kuwa hatua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti huyo wa bodi imesababisha  sintofamu miongoni mwa watumishi wa shirika kuhusu masuala mbalimbali.

Kwa mujibu wa habari za kuaminika kutoka katika shirika hilo, miongoni mwa mambo hayo ni  hatima ya mishahara yao ambayo hawajalipwa kwa zaidi ya miezi minne sasa.

MTANZANIA ilipomtafuta Mzindakaya   kuthibitisha madai ya kujiuzulu kwake, aliomba atafutwe leo ambako atakuwa kwenye nafasi ya kuzungumzia suala hilo.

“Ninaomba nisubiri kesho (leo) utakachokiona,” alisema Mzindakaya.

Alipoulizwa ukweli kuhusu kujiuzulu kwake alisisitiza na kumtaka mwandishi asubiri hadi leo na si vinginevyo.

Kwa miaka kadhaa sasa, NDC   imekuwa ikiyumba huku ukaguzi wa CAG ukimulika miradi yake minne ambayo kwa kiwango kikubwa inamilikiwa na washirika binafsi, zikiwamo gharama za utafiti ambazo hugharamiwa nao kwa kiwango kikubwa.

Ripoti hiyo ya CAG ya 2014/15 ilizungumzia miradi minne kati ya mitano ikiwamo ya Makaa ya Mawe ya Liganga na Mchuchuma   na kilimo cha Mawese.

CAG alisema miradi hiyo ya ubia katika ya NDC na washirika wake haina kumbukumbu ya utafiti aa upembuzi yakinifu katika maeneo mbalimbali ambako miradi ya maendeleo inakusudiwa kuwepo.

“Kukosekana kwa kumbukumbu kunalifanya Shirika la Maendeleo la Taifa kuwa kwenye nafasi ndogo katika majadiliano ya mgawanyo wa rasilimali hivyo kusababisha miradi isitekelezeke bila kugharimiwa na wawekezaji,” ilieleza taarifa hiyo ya CAG.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles