21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

MZEE MAJUTO ALAZWA ICU


MCHEKESHAJI mkongwe nchini Amri Athumani ‘Mzee Majuto’, Jumatano wiki hii alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuzidiwa na kulazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).

Masoud Kaftany ambaye ni kiongozi wa chama cha waigizaji Wilaya ya Kinondoni, ameliambia Swaggaz kuwa Mzee Majuto amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maumivu makali ya miguu na nyonga.

“Kinachomsumbua ni maumivu ya nyonga, mwili na miguu kiasi kwamba amefikia hatua hawezi kutembea na kula. Lakini kingine ni kile kidonda alichofanyiwa upasuaji India bado hakijakauka, kinamwongezea maumivu. Jambo kubwa kwa sasa ni kumuombea,” alisema Kaftany.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles