28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti wa Wazazi CCM Sengerama atoa kadi 1,000

Na Anna Ruhasha, Mwanza

Mweyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Jacksoni Mazinzi ametoa kadi 1,000 za chama hicho kwa ajili ya kupunguza changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa kadi kwa wanachama wa jumuiya hiyo.

Mazinzi ametoa kadi hizo juzi wakati akitekeleza ahaadi yake mbele ya wananchama wa jumuiya hiyo aliyoihaadi wakati akiomba kura ya za ndiyo katika uchaguzi mkuu ndani ya CCM ya kutafuta viongozi katika Jumuiya hiyo.

Aidha, katika uchaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Mazinzi alitangazwa kuwa mshindi na Msimamizi wa uchaguzi huo, Mwashamu Ismail bada ya kupata kura 371

Mazinzi akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua alisema kuwa katika uongozi wake katika kipindi cha miaka mitano atahakikisha anapunguza changamoto zinazozikabili jumuiya hiyo.

“Nimeamua kugombea nafasi hii kwa sababu nimebaini jumuiya hii imekuwa ikikabiliwa na changamoto kama vile uelewa juu ya mambo kadhaa ya jumuiya niwaambie wanachama nitaanza kutoa semina kwenu,” alisema Mazinzi.

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk. Charlse Tizeba ambaye ni mmoja ya wachaguliwa katika uchaguzi huo katika nafasi ya mwakilishi wa mkutano mkuu taifa kupitia jumuiya ya wazazi akizungumza na wapiga kura baada ya kutangazwa kuwa mshindi amesema ataitumikia jumuiya hiyo kwa ufanisi kutokana na uzoefu alionao hasa katika kudumisha umoja kwa wanancha.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani Sengerema, Agustine Makoye amesema uchaguzi ulifanyika ni kwamujibu wa katiba ya chama huku Katibu wa chama hicho wilayani humo, Muksin Zikatimu akisema kuwa uchaguzi ngazi za jumuiya umeisha na kuwataka viongozi waliochaguliwa kwenda kufanya kazi za chama kwa weledi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles