32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti wa Kijiji atumbuliwa kwa ubadhirifu wa Fedha

Mohamed Hamad, Kiteto

Serikali wilayani Kiteto mkoani Manyara imemsimamisha kazi Mwenyekiti wa Kijiji cha Dosidosi, Salmu Mbwegu kwa ubadhirifu wa fedha za wananchi alizokuwa anachangisha mnadani.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumain Magesa, akiwa Kijijini hapo alisema Serikali ya awamu ya tano haiwezi kuvumilia wizi huo ambao umesababisha halmashauri kukosa mapato

“Kiongozi wa Serikali akituhumiwa lazima akae pembeni kwanza mpaka amalize tuhuma yake, mwenyekiti wenu anatuhumiwa kuwa na risiti feki za michango baada ya uchunguzi unaofanywa na Taasis ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) itajulikana ingawa hapa nimepata taarifa ameanza kurejesha Sh. 500,000 kati ya Sh. 1,700,000 alizotuhumiwa nazo, “

Awali mwenyekiti huyo alipewa vitabu vya kukusanya ushuru wa halmashauri mnadani kazi ambayo ilipaswa kufanywa na Afisa mtendaji, badala yake akaanza kukusanya mwenyewe huku akizalisha risiti feki na kuisababishia manung’unuko na malalamiko kwa wananchi.

Kijiji cha Dosidosi huwa kunafanyika mnada mara mbili kwa mwezi hivyo kwa kipindi chote halmashauri ya wilaya imekuwa ikipata mapato kidogo kinyume na  kusudio na kupata hasara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles