Ramadhan Hassan-Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Seleman Sadiqq, amesema ukadirio wa kodi unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na kutokuruhusiwa wafanyabiashara wanaonunua bidhaa China na Dubai kwenda na fedha taslimu umekuwa ni tatizo.
Akichangia mjadala wa Bajeti kuu ya Serikali leo June 18 bungeni Sadiqq amesema tatizo lipo kwenye ukadiriwaji wa kodi na kwamba biashara za Dubai na China zimetawaliwa kwa kulipa fedha taslimu.
“Ni muhimu kwa Benki Kuu (BOT), ueleze utaratibu wa kupeleka fedha taslimu ukoje. BOT wasaidie kuhakikisha biashara inarudi Kariakoo, kwa sasa imepotea katika ramani ya biashara,” amesema.
“Tulikuwa na Kariakoo ya wafanyabiashara kutoka Malawi, Kariakoo, Burundi,
Congo, Uganda na Rwanda, BOT na TRA lazima wajiuelize kuna nini na sababu zipi tulizopoteza
biashara Kariakoo,” amesema.
Aidha Mbunge huyo amesema sera ya Tanzania ya viwanda kwa sasa inatekelezeka
kwa vitendo kutokana na ujenzi wa viwanda unaofanyika katika maeneo mbalimbali
nchini.