24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

MWENYEKITI CCM KIZIMBANI KWA RUSHWA

Na MWANDISHI WETU-ZANZIBAR

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, Haji Ameir Haji, amefikishwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar iliyopo Vuga, akikabiliwa na shtaka la utoaji rushwa, katika kura ya maoni ya chama hicho.

Ameir ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM anadaiwa kutoa rushwa kwa wajumbe katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 pamoja na kuwashawishi wapiga kura kwa kuwapa kofia za kiua na madira kwa lengo la kuwashawishi wampigie kura katika uchaguzi wa kura za maoni kupitia CCM.

Ameir, alifikishwa jana mbele ya Jaji Mukusa Isaac Sepetu, kuendelea na kesi hiyo iliyo katika hatua ya kusainiwa hati ya makubaliano ya hoja zilizokubaliwa na mshitakiwa.

Hati hizo zilisainiwa kwa pamoja na Jaji Mkusa, Mwendesha Mashitaka Anuar Khamis Saaduni, wakili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) pamoja na Wakili wa kujitegemea Abdallah Juma anayemsimamia mshitakiwa katika kesi hiyo.

Baada ya saini hiyo, Jaji Mkusa Isaac Sepetu, aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 19 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa mashahidi wa upande wa mashitaka.

Hata hivyo kada huyo wa CCM alidhaminiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar Ramadhan Abdallah Ali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles