24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanza wachagua Naibu Meya

NA CLARA MATIMO- MWANZA

MADIWANI wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wamemchagua Diwani wa Kata ya Nyamagana, Bikhu Kotecha (CCM), kuwa Naibu Meya wa jiji hilo kwa mara nyingine tena.

Uchaguzi huo ulifanyika katika Mkutano Mkuu wa  mwaka wa fedha wa halmashauri hiyo juzi baada ya Kotecha kumaliza muda wake wa kuongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Agosti mwaka jana.

Akitangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo, Katibu Tawala wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Jonas Madulu, alisema Kotecha ameshinda kwa kura 20 za ndiyo kati ya 21 zilizopingwa na kura moja imeharibika.

“Hakuna chama kingine cha upinzani ambacho kimemteua mgombea zaidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa kusimamia uchaguzi huu, kulingana na kura zilizopigwa, namtangaza Kotecha kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kipindi cha mwaka mmoja (2018/19), ambaye ameshinda kwa asilimia 95.2, kura moja iliharibika,” alisema.

Akiwashukuru madiwani waliomchagua baada ya kutangazwa matokeo, Kotecha alisema ataendelea kushirikiana nao katika kutekeleza ilani ya CCM kuwaletea wananchi maendeleo.

“Nawashukuru sana  kuniamini na kunichagua kushika nafasi hii kwa kipindi cha miaka minne mfululizo, kila mwaka tunapofanya uchaguzi kuanzia mwaka 2016 hadi 2019 mmeniamini na kunipa kura nyingi za ndiyo, na mimi sitawaangusha, nitatimiza wajibu wangu kwa manufaa ya wananchi waliotuchagua,” alisema.

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, James Bwire, alisema kitendo cha vyama vya upinzani kuacha kuteua mgombea katika uchaguzi huo ni kiashiria tosha kwamba vimeridhika na kuunga mkono juhudi za CCM.

“Hivi sasa tunaelekea kwenye uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa, hivyo nawaagiza madiwani wote wa CCM  kufanya mikutano ya hadhara na mimi nitatembelea kata zote nikiwa na wataalamu wa Tarura, Mwauwasa na Tanesco ili wajibu na kutatua  kero za wananchi katika maeneo hayo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles