24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mwandosya kuchukua fomu ya urais Juni tatu

MwandosyaNa Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya, anatarajia kuchukua fomu kuwania urais Juni tatu mwaka huu.

Mwandosya ambaye tayari ametangaza kuacha kuwani ubunge katika Jimbo la Rungwe Mashariki, anakusudia kutangaza nia yake ya kusaka safari ya kuelekea Ikulu, Juni Mosi, mwaka huu.

Akizungumza na Mtanzania jana nje ya viwanja vya Bunge, Profesa Mwandosya alisema sababu zilizomsukuma kuwania urais, atazitaja Juni Mosi atakapotangaza nia mkoani Mbeya.

” Sababu za kutaka kuwania urais na nini nitawafanyia Watanzania, nikiingia madarakani nitaeleza siku ya kutangaza nia Juni Mosi,” alisema Profesa Mwandosya.

Waziri Mwandosya ni mmoja kati ya makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao kwa muda mrefu wameonesha nia ya kutaka kumrithi Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake.

Ikumbukwe kuwa Waziri Mwandosya alipata kuwania urais mwaka 2005 na aliingia kwenye kundi la tatu bora miongoni mwa wagombea 11 waliowania nafasi hiyo.

Walioingia tatu bora mbali ya Profesa Mwandosya ni pamoja na Dk. Salim Ahamed Salim na Rais Jakaya Kikwete ambaye aliibuka mshindi.

Mwandosya amewahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali katika Serikali za awamu tofauti tofauti.

Hatua hiyo ya kutangaza nia imekuja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutangaza ratiba ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho kuanza kuchukua na kurejesha fomu.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, wagombea wa nafasi ya urais muda wa kuchukua fomu ni Juni 3 hadi Julai 2, muda ambao utatumiwa sambamba na kazi ya kutafuta wadhamini mikoani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles