32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mwandishi afikishwa kortini kwa tuhuma za utekaji

Na KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

JAMHURI imemfikisha mahakamani mwandishi wa habari wa Gazeti la Jamhuri, Angellah Kiwia (41) na mwenzake wakituhumiwa kwa mashtaka manne, ikiwemo utekaji nyara.

Angellah na Mohamed Rushaka (36), wamefikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Ester Martine.

Wakili Ester alidai katika shtaka la kwanza, washtakiwa wanadaiwa kati ya Machi mosi na Machi 31, 2020 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, kwa makusudi waliongoza genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

Katika shtaka la pili la utekaji nyara kwa lengo la kudhuru, washtakiwa wanadaiwa siku hiyo katika Jiji la Dar es Salaam, walimteka Seleman Mohamed wakiwa na lengo la kumpeleka katika hatari ya kumuumiza.

Katika shtaka lingine, washtakiwa hao wanadaiwa wakiwa na lengo la kulipwa, walidai kiasi Sh milioni 30 kutoka kwa Seleman Mohamed, huku wakimtishia kumuua.

Shtaka la mwisho la kutakatisha fedha, washtakiwa hao wanadawa katika kipindi hicho walijipatia Sh milioni 30 kutoka kwa Mohamed, huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la makosa tangulizi ya kuratibu genge la uhalifu.

Upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa kesi kutajwa.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote, Hakimu Chaungu aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 25, itakapotajwa na wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili kutokuwa na dhamana

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles