27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanamume aamua kufunga ndoa na maiti kutimiza ahadi

Akimvisha pete
Akimvisha pete

NA JOSEPH HIZA,

DAIMA dunia yetu hii tushimo ni sayari isiyokaukiwa na vituko, vijimambo vya hapa na pale. Na mojawapo ni tukio hili la kushangaza wakati kijana mmoja nchini Thailand alipoamua kufunga ndoa na maiti alikuwa mchumba wake aliyefariki ghafla kutokana na ajali ya gari.

Kijana huyo Chadil Deffy, mwandaaji wa vipindi vya televisheni, akijulikana pia kwa jina la Deff Yingyuen nchini Thailand, alifunga ndoa na msichana wake huyo wa kike akiwa mfu ili tu kutimiza ahadi yake ya upendo.

Akiwa na umri wa miaka 29 na mchumba wake mwenye umri wa miaka 28, Sarinya Kamsook walikuwa wamepanga kuoana kabla ya tukio hilo.

Sarinya kwa bahati mbaya alifariki dunia katika ajali mbaya ya gari, saa sita baadaye kutokana na kupata majeraha makubwa. Ikiwa ni siku moja kabla ya tukio kubwa la harusi yao. Kwa sababu hiyo, Deffy hakuwa na jinsi zaidi ya kuendelea na mipango ya harusi hiyo.

Ibada hiyo ya harusi iliunganishwa na ibada ya mazishi iliyofanyika katika kitongoji cha Surin, Thailand.

Katika mazishi ya binti huyo, Duffy alimvisha pete mpenzi wake huyo marehemu. Na tukio hilo likawa ni la kipekee kutokea hapa duniani likihusisha ibada ya harusi na mazishi kwa wakati mmoja.

“Deffy na Sarinya walikuwa pamoja kwa miaka 10, hatimaye waliamua kukaa chini. Walikuwa wameahirisha harusi mara kadhaa, kutokana na kutokupata muda muafaka na ukweli kwamba Deffy alitaka kumaliza elimu yake kabla ya kufunga  ndoa.

Hata hivyo, baada ya kifo cha mpenzi wake, Sarinya Deffy aliona hakuna kizuizi cha yeye kutimiza shauku yake ya kufunga harusi na mchumba wake huyo, hivyo aliamua kufunya harusi kabla ya kumzika.

Sherehe hiyo ya Kibuddhist  ilifanyika katika mji wa Surin kaskazini mwa Thailand.

Deffy alisema mbele ya jamaa na marafiki waliokuwapo katika sherehe kuwa ibada hiyo amefanya ili kuonyesha upendo wake mkubwa  kwa Sarinya.

Aidha, badaye katika ukurasa wake wa Facebook alisema: katika macho yenu, matendo yetu yanaweza kuonekana kama tuliokuwa katika upendo mkubwa.

“Lakini kwetu sisi, ni makosa ambayo hatungeweza kuyarudisha nyuma ili kuyasahahishia. Kumbuka maisha ni mafupi mno.

“Fanya unachopenda na jali watu unaowapenda, wawe wazazi wako, ndugu zako. Unaweza usipate fursa tena,” alisema.

Marafiki na jamaa kadhaa walihudhuria harusi hiyo na tukio hilo lilivuta hisia za watu wengi nchini humo na kufanya TV ya taifa ya nchi hiyo kurusha tukio moja kwa moja. Simulizi, pamoja na picha kutoka kwenye harusi hiyo sasa vimevuta hisia za watu wengi katika mitandao, hivyo kuzua mijadala kadhaa.

Mwandaaji huyo wa televisheni alikutana na marehemu huyo wakiwa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Mashsariki Mwa Asia. Wamekuwa pamoja kwa miaka 10 na walizungumzia ndoa yao mara kwa mara, hii ni kwa mujibu wa gazeti la kila siku nchini humo Pattaya News.

Katika mazishi, mashada ya maua yaliwekwa na marafiki na ndugu pamoja na waigizaji na waimbaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles