24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanamke awanywesha wakwe zake chai ya mkojo

684aeb2-69130-fotorcreated65464-0d0200000-0d0588235-0d9840000-0d9444444-sector_668x376-crop

FARAJA MASINDE NA MITANDAO

DUNIA ina mambo na mambo yenyewe ndiyo haya! Mwanamke mmoja nchini India, Rekha Nagvanshi (31) amejenga tabia ya kukojolea vikombe vya wakwe zake kila siku kwa muda wa mwaka mmoja.

Kama wasemavyo Waswahili kuwa za mwezi ni arobaini, ndicho kilichomkuta mwanamke huyo, Rekha baada ya kufumwa na mama mkwe wake jikoni akikojolea ndani ya  chupa ya chai.

Sababu ya yeye kufanya hivyo inasemekana kuwa ni kitendo cha wakwe zake hao kumpiga marufuku mtoto wao Deepak Nagvanshi

(34) ambaye ni mume wa Rekha kufanya kazi za nyumbani kwa kuwa mkewe yupo.

Kitendo hicho kilimchukiza dada huyo hivyo akaamua kutumia njia hiyo ya kuwanywesha mkojo wakwe zake, ambapo alikuwa akikojoa kwenye vikombe wanavyonywea chai na chupa ya chai wakati mwingine ikiwa na chai ndani yake, alifanya hivyo kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi alipokuja kukamatwa.

Rekha na mumewe walikuwa wakiishi nyumba moja na wakwe zake, katika Wilaya ya Indore Jimbo la Madhya Pradesh, nchini India.

Rekha anasema kuwa ingekuwa jambo la busara zaidi kwake yeye kuishi na ndugu zake kuliko kuishi kwa wakwe zake hao.

Anasema hakuwahi kuwa na furaha kutokana na namna alivyokuwa akiishi kwenye ndoa yake hiyo.

Anasema maisha ndani ya nyumba hiyo yalimfanya ajihisi kama hatendewi haki, ikiwamo kutopata matunzo stahiki kama wanawake wengine waliopo kwenye ndoa.

Akizungumzia maisha ya ndoa ya Rekha, rafiki yake Alia Kohli (33), anasema hakuwahi kumuona akiwa na furaha na ndoa yake tangu siku ya kwanza ya harusi yao.

Anabainisha kuwa mumewe alikuwa akimfanya kama mtumwa.

Anasema kabla ya kuanza kuishi na wakwe, walikuwa wakiishi wenyewe lakini mume hakumpa heshima yake anayostahili, hivyo alilazimika kuomba kurudi kwa wazazi wake kwa kuwa mambo yalikuwa yamemfika shingoni.

Hata hivyo, jambo la kushangaza baada ya kurejea kwa wazazi wake, Rekha aliomba kurejea ukweni kwa madai kwamba alikuwa akihitaji kuwa karibu na kumlea mwanawe aliyekuwa na umri mdogo wa miaka minne, ambaye tangu awali alikuwa akiishi na wakwe zake.

Mara baada ya kuanza maisha mapya ukweni, alimpa mumewe masharti kuhakikisha anampikia chakula, anamfanyia masaji na kumfulia nguo zake zote.

Wazazi wa mwanamume hawakuridhishwa na masharti hayo, hivyo waliweka mpango wa kumkomesha.

Baada ya wakwe kumwekea ngumu, Deepak ambaye ni mumewe alisema kuwa yupo radhi kufuata masharti ya mkewe, lakini wazazi wake walimjia juu na kusema kwamba hiyo haikubaliki kwani anamshurtisha mtoto wao na kumfanya kama mtumwa.

Licha ya kuishi katika nyumba moja, wakwe walikuwa wakijitegemea kwa kila kitu, yaani Rekha na mumewe walikuwa wakipika wenyewe chakula chao na wakwe zake walijitegemea.

Lakini, wazazi hao walikuwa na utaratibu wa kuwatembelea watoto wao mara moja kwa wiki ili kuona namna ambavyo mtoto wao anatumikishwa.

Kitendo hicho pia kilichangia kwa asilimia kubwa mwanamke huyo kuweka utaratibu wa kuwanywesha chai iliyochanganywa na mikojo.

Baada ya wazazi kugundua mchezo huo mchafu, walisema kwamba walijua mkwe wao hawapendi lakini hawakuwahi kufikiria kama anaweza kuchukua uamuzi mgumu kiasi hicho.

“Hatukuwahi kufikiria kama mkwe wetu anaweza kutunywesha mikojo, kwani alikuwa akitabasamu na kutukaribisha chai kwa ukarimu wa hali juu, nasi tuliipokea kwa moyo wote tukitambua kuwa anatukarimu,” anasema Suraj Nagvanshi.
Mwanamke huyo akijiandaa kujisaidia haja ndogo.
Mwanamke huyo akijiandaa kujisaidia haja ndogo.

Anasimulia kuwa siku aliyomkuta mkwewe akikojolea kwenye birika la chai, hakuamini macho yake.

Anasema wao waliingia ghafla jikoni kwa mkwe wao, hivyo hakujua kama wanaweza kumuona.

“Tuliamua kwenda kutoa taarifa polisi, tukaambiwa masuala ya namna hiyo hawashughuliki nayo. Lakini sisi tunataka sheria ichukue mkondo wake maana hiki tulichofanyiwa si jambo jema… yaani mtu amekuwa akitunywesha mikojo kwa muda wa mwaka mmoja sasa, halafu aachiwe hivi hivi… haiwezekani, ni lazima haki itendeke,” anasema mama huyo.

Aidha, familia hiyo imeamua kufungua shauri mahakamani. Rekha na Deepak nao iliwalazimu kutengana maana kitendo walichofanyiwa wazazi wake hakikuwa cha kufumbiwa macho.

Hiyo ndio dawa ya wakwe wakorofi, ukimuudhi mkweo jiandae kula chakula ama chai yenye mikojo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles