23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanafunzi Darasa la sita akutwa amejinyonga Morogoro

Na Ashura Kazinja, Morogoro

 Mwanafunzi wa Darasa la sita shule ya msingi Lukobe, Egdilus Edmundi  (13) mkazi wa mtaa wa Tushikamane kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro, amekutwa amejinyonga Hadi kufa chumbani kwa dada yake  kwa kutumia kamba  ya manila (nailoni) aliyoifunga kwenye kenchi.

Dada wa marehemu, Editha Edmundi ambaye alikua mtu wa kwanza kushuhudia tuko hilo amesema siku ya tukio marehemu alikataa kwenda kanisani akidai anamalizia kazi za shule (homework), hivyo dada yake alienda kanisani na baba yake alienda kazini, baadae aliporejea nyumbani majira ya saa nane mchana, alimkuta mdogo wake ananing’inia juu ya paa akiwa tayari amefariki 

Nae baba wa marehemu  Edimund Peter ameeleza kuwa mwanawe hakua na tatizo la akili na alikua mtu mwenye furaha muda wote hivyo tukio hilo linawapa maswali mengi kujua ni nini  kilichomsibu kijana wao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo wa Tushikamane, Omary Hassan amesema Kuna haja ya wazazi kuwa karibu na watoto wao ambapo amesema huenda familia hiyo kuishi na baba yao peke yake huku Mama yao akiwa anaishi sehemu nyingine imekua sababu ya kutofahamika chanzo cha kifo chake, kutokana na mtoto huyo kukosa sehemu ya kufikisha changamoto zinazomkabili.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu, Kamanda wa polisi mkoa Morogoro Fortunatus Musilimu, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema tukio hilo limetokea novemba 14 mwaka huu katika mtaa wa Tushikamane kata ya Lukobe  na kuongeza kuwa Hadi  sasa uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo bado unaendelea.

“Hakuna watu wanaoshikiliwa kwa tukio hili, na marehemu hajaacha ujumbe wowote, hivyo uchunguzi unaendelea,” ameeleza Kamanda Musilimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles