24.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mwalimu Mkuu akamatwa kwa kumpiga mwanafunzi Kagera

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Charles Mkaruka (33), Mjita Mkristo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kiteme, iliyopo Kijiji cha Kiteme, Kata ya Kasharunga, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba, kwa kosa la kumshambulia Filinet Augustino (18), mwanafunzi wa kidato cha tatu, baada ya kukataa kusoma somo la Fizikia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda, alitoa taarifa hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari mjini Bukoba. Chatanda alisema tukio hilo lilitokea Julai 3, 2024, majira ya saa nane mchana katika Shule ya Sekondari Kiteme. Mtuhumiwa alishambulia mwanafunzi huyo kwa kumpiga fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake akiwa darasani na wanafunzi wenzake.

“Mwanafunzi huyo anaendelea na matibabu katika Kituo cha Afya Kimeya baada ya kushambuliwa na mtuhumiwa,” alisema Chatanda.

Mwanafunzi aliecharazwa na mwalimu wake baada ya kuonyesha hawezi kusoma somo la mwalimu huyo.

Chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa kushindwa kuzuia hasira na kutoa adhabu iliyopitiliza kwa mwanafunzi huyo, hadi kufikia hatua ya kumkimbiza kituo cha afya kwa huduma ya kwanza.

Chatanda aliongeza kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea kushirikiana na taasisi ya elimu ili kupata ukweli wa chanzo cha tukio hilo. Aidha, aliwasihi watumishi wote wa idara ya elimu kutekeleza majukumu yao kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na idara hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Abell Nyamahanga, alisema mwalimu huyo amevuliwa madaraka ya kuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kiteme kutokana na tuhuma zinazomkabili za kumuadhibu na kumsababishia majeraha mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu, ili kupisha uchunguzi.

“Hatua hii ni muhimu ili kuhakikisha uchunguzi unafanyika kwa uwazi na haki,” alisema Nyamahanga.

Tukio hili limeibua mjadala mkali kuhusu matumizi ya adhabu kwa wanafunzi shuleni, na umuhimu wa kufuata taratibu za kisheria na kitaaluma katika kushughulikia matatizo ya nidhamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles