26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mwakinyo atamba yuko fiti asilimia 98 kupanda ulingoni Zanzibar

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya pambano lake dhidi ya Mbiya Kanku litakalofanyika Januari 27, 2024 Bondia wa Hassan Mwakinyo amesema amekamilisha maandalizi kwa asilimia 98 kilichobaki ni kupima uzito pekee.

Mwakinyo na Kanku raia wa DR Congo wanatarajiwa kupanda ulingoni katika pambano la ubingwa wa WBO Afrika litakalopigwa Amani Complex Indoor Arena, Zanzibar.

Mwakinyo amesema amejiandaa kila idara, hivyo mpizani hata akimjia kwa mtindo gani yupo tayari kupambana naye, kwani mikono ndiyo itaongea ulingoni.

Bondia huyo mwenye jina kubwa nchini, amewatoa hofu mashabiki wa masumbwi visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuwa siku hiyo ataonesha burudani ya kuvutia ya ngumi.

Mapambano mengine yatakayopigwa siku hiyo, Hussein Itaba dhidi ya Juma Misumari wa Morogoro, Bakari H.Bakari na Seleman Hamad, Masoud Khatibu atazichapa na Yahaya Khamis, huku mwanadada Zulfa Iddi akivaana na Debora Mwenda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles