Kiwango cha joto kwa mwaka 2016 kimeweka rekodi yakuwa ni mwaka wa joto zaidi ukilinganisha na miaka ilyopita kama vile 2015.
Kwa mujibu wa tawkimu kutoka Shirika la Anga la Marekani (NASA) na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza (UK Met Office) zimeainisha hali ya joto kidunia imeongezeka mara dufu mwaka 2016 kutokana na dunia kukumbwa na kipindi cha El Nino.
Kwa mujibu wa wanasayansi, El Nino ni hali ya kuongezeka kwa joto kwenye mstari wa Ikweta katika bahari ya Pacific, kipindi ambacho kinakadiriwa kuwa hujirudia kila baada ya miaka 5, hali hii ilianza kushuhudiwa katikati ya mwaka jana. Hii ni moja ya athari za mabadiliko ya tabia nchi pia.