Na Denis Sinkonde, Songwe
Zaidi ya nyumba 19 zimebomolewa na nyingine saba zimeezuliwa mapaa na nyingine zimebomolewa kuta huku mifugo kama vile mbuzi na kuku kusombwa na mafuriko baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kunyesha katika Kijiji cha Chilulumo wilayani Momba mkoani Songwe.
Akizungumza eneo la tukio baada ya maafa hayo kutokea Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Momba ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Anna Gidarya amesema maafa hayo yametokea Februari 11, 2022 usiku katika kijiji cha Chilulumo kata ya Chilulumo wilayani humo ambapo nyumba 19 zimebomolewa na nyingine saba kuezuliwa na upepo mkali.
“Tumetuma timu ya wataalamu kufanya tathimini ya majengo ili kujua hasara madhara yaliyotokea kutokana na maaafa hayo ikiwamo mifugo na vyakula vilivyoharibika vingine kusombwamamaji,” amesema Gidarya.
Aidha, Gidarya amewasihi wananchi wa kijiji cha Chilulumo kushirikiana na serikali kwa kuwasaidia wahanga hususan kuwasaidia sehemu za kulala, chakula pamoja na mahitaji mengine wakati serikali ikiwa inaendelea na tathimini.