30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Muswada wa jinsi walivuruga Bunge Kenya

Nairobi, Kenya



Wanasiasa wa Kenya wanapaswa kupitisha muswada wa jinsia ambao utahakikisha theluthi moja ya viti katika bunge ni maalumu kwa wanawake, kuliko hatari ya kuifanya nchi kuwa na mgogoro wa kikatiba, wabunge wanaounga mkono hoja wameonya.

Licha ya katiba ya mwaka 2010 kueleza kuwa hakuna zaidi ya theluthi mbili ya kikundi chochote kilichochaguliwa au kuteuliwa kinaweza kuwa na jinsia moja, huku wanawake wakiwa na asilimia 22 ya viti katika nyumba ya chini ya bunge, na asilimia 31 katika nyumba ya juu.

Maamuzi ya mahakama tangu mwaka 2012 yamesababisha bunge kupitisha sheria kutekeleza muswada wa jinsia au hatari ya kufutwa,  lakini majaribio ya awali yameshindikana na wabunge wa kike wakihukumu wabunge wa kiume kwa kuzuia juhudi hizo kwa makusudi.

Ikiwa bunge litagawanyika na kuvunjika, uchaguzi mkuu utaitishwa. Pamoja na uchunguzi uliofanyika kutoka kwa mahakama, nyumba ya chini ya Kenya inatarajiwa kupiga kura kwenye muswada Jumatano.

Naye mwakilishi wa wanawake wa Kisumu na Makamu wa Rais wa Umoja wa Wanawake wa Bunge la Kenya, Rozaah Buyu, ameongelea juu ya sakata hilo kuonekana ni kinyume na Katiba ya Kenya

“Kweli ni kinyume na katiba, lakini je, ni mamlaka gani tunayowaletea watu wengine wakati hatufanyi kazi ndani ya katiba kwa kupuuza utawala wa kijinsia?

“Mahakama ya juu mwaka 2017 imesema kuwa Jaji Mkuu anaweza kumshauri rais kufuta bunge kama sheria haijatayarishwa,”  amesema Buyu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles