24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Museveni aendelea kukaza masharti ya corona

 KAMPALA, UGANDA

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amesema shule, makanisa, misikiti, vilabu, vilabu vya usiku, maeneo ya kufanyia mazoezi na saluni za urembo zitaendelea kufungwa ili kuepuka maambukizi ya virusi vya corona.

Museveni alisema si rahisi kwa maeneo hayo kufuata masharti ya kutochangamana na kwamba muda wa kuwa ndani ya nyumba utaendelea kuwa kuanzia saa moja usiku hadi saa 12:00 kwa siku 21 zaidi.

Makanisa, vilabu vya pombe, vilabu vya usiku, maeneo ya kufanya mazoezi na sauna yataendelea kufungwa kwa siku 21, huku kufungua shule kwa wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani kukiwa kumeahirishwa wakisubiri kwa mwezi mmoja. 

‘’Tumeamua kuahirisha kufunguliwa kwa shule kwa wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani kwa mwezi mmoja zaidi tukijiandaa zaidi na kutazama hali ilivyo,’’alisema Museveni. 

Wenye magari ya dalala wamemaliza miezi miwili na nusu bila kazi tangu marufuku ilipowekwa mwezi Machi.

“Kuanzia tarehe nne nitaruhusu kuanza tena kwa usafiri wa umma wa mabasi, usafiri wa abiria wa treni na dalala kuchukua abiria nusu,’’ alisema Museveni.

Viwanja vya ndege vitaendelea kufungwa pia magari binafsi hayataruhusiwa kufanya kazi katika maeneo ya mpakani

Mwezi Machi Rais Museveni alitangaza kufunga taasisi za elimu, mikusanyiko nchini Uganda na kuzuia raia wa Uganda kusafiri kuelekea nchi zilizo na maambukizi ya virusi vya corona.

 Raia wa Uganda wanaowasili kutoka nje wanatakiwa kujiweka karantini kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe.

Museveni aliamuru kufungwa kwa shule za msingi, sekondari na taasisi za elimu ya juu kuanzia Machi 20, kwa muda wa mwezi mmoja, lakini sasa muda huo umeongezwa.

Mikusanyiko ya umma ikiwemo mikutano, mikutano ya uchaguzi, mikutano ya kawaida ya kitamaduni pia imepigwa marufuku.

Wakati huo huo Rais Museveni amesema kuwa itakua ni uendawazimu kuendesha uchaguzi wakati wa mlipuko wa virusi vya corona. 

Aliliambia shirika la habari la Uganda NBS kwamba mipango ya kufanya uchaguzi mapema mwaka 2021 haitakuepo kama virusi vya corona havitadhibitiwa.

Mikutano ya umma ikiwemo ya kisiasa imepigwa marufuku kama sehemu ya hatua za kutosogeleana na kukaa nyumbani zilizowekwa nchini humo kwa ajili ya kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona.

Takriban wagombea 24 wametangaza nia ya kugombea kiti cha urais na wamewasilisha maombi yao kwa Tume ya Uchaguzi ili kukabiliana na Rais Museveni na wameanza mikutano ya kitaifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles