24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Kauli ya Trump yaongeza ghadhabu ripoti mpya kifo cha Mmarekani mweusi ikitoka

 WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump, ametishia kutumia nguvu zote za vyombo vya ulinzi vya kijeshi na vya kiraia kusimamisha ghasia zilizozuka baada ya kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd. 

Wakati Trump akisema hayo, uchunguzi mpya uliofanywa kwenye mwili wa Floyd aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi, umedhihirisha kuwa kifo chake kilitokana na kukosa pumzi kutokana na kukabwa koo kwa goti na ofisa wa polisi mzungu. 

Matokeo ya uchunguzi huo mpya ulioidhinishwa na familia yake, yanakinzana na yale ya uchunguzi wa awali, ambao ulisema Floyd alikufa kutokana na matatizo ya kiafya ambayo tayari alikuwa nayo. 

Ripoti ya uchunguzi huo imeibua upya madai ya kutaka hatua zaidi kwa maofisa wengine watatu waliosimama na kutazama tu wakati mwenzao Derek Chauvin alipomkandamiza kwa goti Floyd. 

Kaka yake marehemu aliyekuwepo wakati ripoti hiyo mpya ikitangazwa, ametoa ujumbe wa kutaka maandamano yote yafanyike kwa njia ya amani. 

Ilitarajiwa kuwa ofisa anayetuhumiwa kumuuwa Floyd angefikishwa kizimbani juzi, lakini mahakama ilisema shughuli hiyo imeahirishwa hadi Juni nane.

Juzi jioni, Rais Trump, atishia kutumia nguvu zote za vyombo vya ulinzi vya kijeshi na vya kiraia kusimamisha ghasia zilizozuka baada ya kifo cha Floyd. 

Trump alisema ikiwa magavana wa majimbo hawatoweza kuhakikisha usalama, atatumia nguvu za kijeshi.

Kuhusiana na ghasia zilizojitokeza katika maandamano ya kupinga ukatili wa polisi, Trump aliahidi kupeleka maelfu ya wanajeshi na silaha nzito mjini Washington, akizitaja ghasia hizo kuwa vitendo vya kigaidi.

Wakati hayo yakijiri, polisi mjini Washington wametumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya watu waliokuwa wakiandamana kwa amani katika bustani ya Lafayette mkabala na Ikulu ya White House. Helikopta zilionekana zikiruka kima cha chini katika anga la mji mkuu huo wa Marekani.

“ Raia wote wa Marekani wameshtushwa na kifo cha George Floyd, lakini kumbukumbu hiyo haistahili kuondolewa na raia wenye ghadhabu, napeleka maelfu na maelfu ya wanajeshi wenye silaha, maafisa wa jeshi na maafisa wa utekelezaji sheria kusitisha uporaji, ghasia, mashambulizi na uharibifu wa mali unaoendelea,” alisema Trump. 

Trump aliongeza kwamba ‘’ikiwa mji au jimbo litakataa kuchukua hatua stahiki, nitapeleka jeshi na kutatua tatizo hilo tena kwa haraka. Nataka wanaopanga ugaidi huu watambue kwamba mutakabiliana na makosa kadhaa ya uhalifu.”

Kauli ya Trump ilikoselewa na mgombea mtarajiwa wa Democrats, Joe Biden, akisema Trump anatumia jeshi la Marekani dhidi ya raia wa Marekani. “Rais huyu anaweza kujidunisha kiasi gani? Matendo yake yanaonesha uhalisia wake,”alisema.

Floyd, raia mweusi wa Marekani ambaye kifo chake kimesababisha maandamano makubwa Marekani, alikufa kutokana na ukosefu wa hewa safi ya (oksijeni), kwa mujibu wa uchunguzi binafsi wa maiti yake.

Alifariki kwa kukandamizwa kwa goti shingoni na mgongoni na maafisa wa polisi wa Minneapolis, uchunguzi wa kimatibabu uliosimamiwa na familia ya Floyd umebaini hilo.

Matokeo hayo yanatofautiana na matokeo ya uchunguzi wa mwili wake uliofanywa na madktari wa mji wake. Matokeo hayo ya awali yalionyesha hakukupatikana ushahidi unaohusisha ukosefu wa hewa wala kunyongwa.

Matokeo ya uchunguzi huo wa kimatibabu pia yalibaini matatizo ya afya yalichangia pakubwa kifo cha Floyd.

Lakini madaktari waliosimamiwa na familia ya Floyd walibaini kifo cha Floyd kilikuwa ni mauaji.

“Sababu ya kifo kwa maoni yangu kimesababishwa na ukosefu wa hewa, kutokana na kukandamizwa shingoni ambako kunaweza kutatiza oksijeni inayokwenda kwenye ubongo na kupelekea mkandamizo mgongoni, ambako kuna tatiza upumuaji,” Dk. Michael Baden, aliyekuwa daktari wa Mji wa New York na mwengine wamesema katika mkutano na wanahabari.

Dkt. Baden alisema hakuwa na tatizo jingine lolote la afya ambalo huenda lingesababisha au kuchangia kutokea kwa kifo chak”.

Matokeo ya uchunguzi huo yana hitilafiana na yale ya uchunguzi wa awali yaliyojumuishwa kwenye malalamishi ya uhalifu dhidi ya Chauvin, ambaye ameshtakiwa kwa mauaji ya kiwango cha tatu na kuua bila kukusudia.

Zaidi ya miji 75 imekumbwa na maandamano kwasababu ya kifo cha Floyd, mitaa ikiwa imefurika watu wanaoandamana bega kwa bega siku chache tu baada ya mitaa hiyo kuwa bila hata mmoja kwasababu ya ni virusi vya corona.

Tukio la kuuawa kwa Floyd limesababisha hasira kwa jinsi maafisa wa polisi wanavyotekeza mauaji dhidi ya raia weusi ni na vitendo vya ubaguzi wa rangi. 

Mauaji hayo yanafuatia yale ya Michael Brown huko Ferguson, Eric Garner, New York na wengine ambako kumepelekea kuanzishwa kwa vuguvugu la ‘Maisha ya mtu mweusi pia ni muhimu’ 

Jumatatu, Rais Trump aliwaambia magavana wa majimbo kwamba wamelegeza kamba mno na wakati unawadia wa kuchukua hatua stahiki na kutumia vizuri vikosi kutoka Jeshi la Taifa, ambapo maelfu yao tayari wamepelekwa katika majimbo mawili.

 “Munatakiwa kukamata watu, munatakiwa kutafuta watu na kuwafunga gerezani kwa miaka 10 na hamtawahi kushuhudia tena kitu kama hiki,” Trump alisema katika mkutano wa njia ya video.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles