28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Muhimbili yaishiwa damu

BloodBanks-628x350Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu na kwa siku wanakusanya chupa 25 hadi 45 pekee, wakati mahitaji halisi ni chupa 70 hadi 100.

Akizungumza na MTANZANIA hospitalini hapo jana, Ofisa Uhusiano wa MNH, Neema Mwangomo, alisema upungufu huo ni sawa na asilimia 60.

“Mahitaji ya damu hapa hospitalini ni makubwa, tunakabiliwa na upungufu kwa asilimia 60. Ili yatosheleze tunahitaji kukusanya chupa 70 hadi 100 kwa siku lakini huwa tunapata chupa 25 hadi 45 peke yake,” alisema.

Mwangomo alisema makundi ya wagonjwa wanaohitaji zaidi kuongezewa damu ni watoto, wajawazito, wagonjwa wa saratani na wagonjwa wa dharura, wakiwamo wale wanaofikishwa hapo baada ya kupata ajali.

“Ili kukabiliana na changamoto hii, hivi sasa tunaendesha mpango wa uchangiaji damu, tunashukuru wapo wananchi wanaojitokeza lakini bado tunawaomba wananchi, taasisi, kampuni binafsi na umma waje kwa wingi ili kwa pamoja tuwasaidie wenzetu wenye uhitaji,” alisema.

Mmoja wa wananchi waliofika hospitalini hapo jana kujitolea damu, Abel Shuma, aliomba watu kujijengea tabia ya kujitolea damu ili kuokoa maisha ya wengine.

“Binafsi nilipopata taarifa hiyo nilijitathmini na nikachukua uamuzi wa kuchangia damu ili na mimi niweze kuchangia ikasaidie kuokoa maisha ya wengine,” alisema.

Naye Flora Manyanga aliwashauri wanasiasa kutumia majukwaa yao, hasa kipindi hiki cha kampeni za Uchaguzi Mkuu kuhamasisha wananchi wakajitolee damu bila kujali itikadi zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles