24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

MUGABE: WALIOWAUA WAZUNGU HAWATASHTAKIWA

HARARE, ZIMBABWE

RAIS Robert Mugabe, ameuambia umati wakati wa sherehe za siku ya mashujaa mjini hapa Jumatatu wiki hii kuwa watu waliowaua wakulima wa kizungu wakati wa mabadiliko ya sheria ya ardhi nchini Zimbabwe hawatashtakiwa.

“Ndiyo, tuna wale waliouawa wakati wakipinga ukoloni. Hatuwezi kuwashtaki wale waliowaua wazungu. Je, tutawashtaki vipi?” alisema Mugabe.

Wakati wa ukoloni, ardhi nzuri ilitengwa kwa wazungu, lakini mwaka 2000, Mugabe aliongoza kutwaliwa kwa ardhi hiyo kutoka kwa wakulima 4,000 wa kizungu.

Rais Mugabe awali alikiri kuwa mifumo ya ardhi ya nchi hiyo ilishindwa na mwaka 2015 alisema: “Nafikiri mashamba tuliyowapa watu wetu ni makubwa, hawawezi kuyasimamia.”

Kutwaliwa ghafla mashamba kutoka kwa wakulima wazungu, inaonekana kuwa sababu kuu ya kuporomoka kwa uchumi wa Zimbabwe tangu mwaka 2000

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles