24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Muethiopia kuinoa Twiga Stars

TWIGASTAANA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), linatarajia kumuaga kocha wa timu ya Taifa ya soka ya wanawake ‘Twiga Stars’, Nasra Abdallah, huku nafasi yake ikitarajiwa kuchukuliwa na Muethiopia, Asrat Abate ambaye anatarajia kutua nchini kesho au Jumamosi.

Abate atarithi mikoba ya Nasra aliyefeli kuing’arisha Twiga, ambayo mapema mwaka huu ilitolewa na Zimbabwe katika mechi za kusaka tiketi ya kushiriki katika fainali ya Mataifa ya Afrika kwa wanawake, zinazotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu nchini Cameroon.

MTANZANIA ilipata habari kutoka nchini Ethiopia, zikidai kuwa tayari TFF ilifanya mawasiliano na Abate kumueleza nia ya kumtaka aje kuifundisha timu hiyo iwe na mafanikio.

“Shirikisho la Tanzania ‘TFF’ linawania kumchukua kocha wetu anaitwa Asrat Abate, alikuwa anafundisha timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 17 na 20, ni mzuri atawasaidia tayari taarifa zimeenea kwetu,” kilisema chanzo hicho nchini Ethiopia.

MTANZANIA baada ya taarifa hizo lilifanya mawasiliano  na ofisa mmoja wa ngazi za juu ndani ya shirikisho, ambaye alikiri kuwepo kwa habari hizo ila kwa sharti la kutotajwa gazetini kwa kuwa sio msemaji.

“Ni kweli aisee, ila umenishtua mmepataje taarifa hizi, kocha anatarajia kuingia nchini Ijumaa au Jumamosi,” alisema kwa kifupi mtoa taarifa huyo.

Nasra alirithi mikoba ya Rogasian Kaijage, ambaye aliamua kubwaga manyanga, awali timu hiyo ilikua inafundishwa na Boniface Mkwasa ambaye kwa sasa anafundisha Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles