25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mtuhumiwa amng’ata mdomo askari

Dar es Salaam
Eneo la katikati ya Jiji la Dar es Salaam

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

KARANI wa Kampuni ya Mabasi ya abiria yaitwayo Happy African, Eliud Mwanyonga (40), amemng’ata mdomo askari wa kikundi cha ulinzi shirikishi aliyefahamika kwa jina moja la Ernest.

Tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita saa 12 alfajiri katika Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani wakati askari huyo alipokuwa katika shughuli zake za kila siku.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, James Zebedayo, aliliambia MTANZANIA Jumatatu kwamba, askari huyo aling’atwa mdomo baada ya kutaka kumkamata Eliud kwa kosa la kutovaa sare za kazi.

“Hawa mgambo walikuja asubuhi walikuwa kama sita hivi na walipofika hapa wakawa wamemuuliza kwanini hakuwa na sare.

“Yeye akawajibu siku hiyo ilikuwa ni Siku ya Mashujaa, kwa hiyo hakuwa na sababu ya kuvaa sare.

“Alipojibu hivyo yule askari wakachachamaa, wakasema lazima amkamate ili akaadhibiwe kisheria lakini yule mfanyakazi akakataa akasema hawezi kukamatwa mara mbili kwa kuwa alikuwa amekamatwa siku chache zilizopita kwa kosa lile lile.

“Baadaye huyo mtuhumiwa alifanikiwa kuwakimbia lakini askari hao walimkimbiza na walipomkamata, walimpiga kwa kutumia fimbo walizokuwa nazo. Walipokuwa wakimpiga, mtuhumiwa naye alijitetea na mwishowe akamng’ata askari huyo mdomo wa chini na kuuondoa kabisa,” alisema Zebedayo.

Kutokana na tukio hilo, askari wengine walifanikiwa kumdhibti mtuhumiwa huyo na kumpeleka katika Kituo cha Polisi kilichoko kituoni hapo kabla ya kupelekwa Kituo cha Polisi Magomeni ambako alifunguliwa jalada lenye namba MAG/RB/7172/2014.

Naye Mkuu wa Kituo cha Polisi Ubungo, Suphiani Masanga, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo ingawa hakutaka kulizungumzia zaidi kwa alichosema kuwa yeye siyo msemaji wa Jeshi la Polisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles