27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mtambo mafuta mazito wazimwa Ludewa, Sh bilioni tisa kuokolewa

Na Elizabeth Kilindi – Njombe


SHILINGI bilioni tisa zitaokolewa baada ya kuzimwa kwa mitambo ya umeme wa mafuta mazito nchini kutokana na kukamilika kwa miradi mikubwa ya umeme wa maji kupitia kituo cha kusambaza umeme cha Makambako-Songea.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, alipozima mtambo wa umeme unaotumia mafuta mazito uliopo Ludewa, Njombe na kuwasha umeme wa gridi ya taifa uliounganishwa kutoka Kituo cha Madaba.

Alisema mradi wa umeme wa Makambako-Songea uliogharimu zaidi ya Sh bilioni 216 utasababisha mitambo inayotumia umeme wa mafuta mazito katika wilaya za mikoa ya Njombe na Ruvuma kuzimwa na kuokoa Sh milioni 897 kwa mwezi.

“Kituo hiki kilikuwa na mashine ya kutumia mafuta mazito yenye uwezo mdogo, ilikuwa na uwezo wa megawati 0.5, kwa mtambo huu peke yake tulikuwa tunatumia zaidi ya Sh milioni 75 kwa kuwasha na kuzima kwa mwezi katika Wilaya ya Ludewa,” alisema Kalemani.

Awali akiwa Kijiji cha Ngalawale kitakachonufaika na mradi huo, alisema vijiji vyote 77 vya wilaya hiyo vitakuwa vimepatiwa huduma ya umeme ifikapo Aprili mwakani.

Aliwataka watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kujipanga na kuhakikisha hakuna kukatika umeme Ludewa.

“Watendaji niwaambie kuanzia wa kufagia, sitavumilia kumwacha mtu yeyote ama meneja, mhandisi au huduma za mteja kutotoa huduma nzuri kwa mwananchi wa Ludewa, sitapenda kusikia umeme unakatikatika,’’ alisema Kalemani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles