RAYMOND MINJA IRINGA
Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa amewaagiza viongozi wote wa kanda hiyo kuanza mikutano ya kisiasa mara moja kwani muda alioruhusu rais umewadia.
Akizungumza kwenye mkutano wake wa kibunge mjini iringa Msigwa amesema chama chao kimejipanga kuanza mikutano ya hadhara kwani muda umedia wa kufanya siasa hivyo viongozi wote wafuate taratibu za kuandika barua za kuandaa mikutano ya hadhara .
Amesema kuwa licha ya katazo la kutofanya siasa lilikuwa ni batili lakini kama chama walitafakari na kuamua kutii agizo hilo ili kusubiri muda aliotangaza rais uwadie na sasa wamejipanga kupiga siasa ya nyumba kwa nyumba, Kijiji kwa Kijiji ili waweze kushinda kwa kishindo na kwenda kushika dola.
“Si alituambia tuache siasa na tusubiri hadi 2020 ndio tuanzee sasa muda umewadia nikufanya siasa kwa kwenda mbele hakuna kulala mpaka kieleweke au mnasemaje makamanda tuliamshee dude,” amesema Msigwa.
Hata hivyo ameitaka serikali kubadili mitaala ya elimu nchini ili wasomi wanapomaliza masomo yao waache kuzunguka na vyeti mitaani kutafuta ajira kutokana na elimu waliyopata imeshindwa kuwaandaa kukabiliana cha changamoto za ajira.
“Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana mitaani wamekuwa wakizunguka kila kukicha kutafuta ajira hadi viatu vinaisha soli kwa kuwa mitaala iliyopo haikuwanda kisaikolojia namna ya kujitegemea na kukabiliana na changamoto za mtaani jambo ambalo limezidi kuwafanya kuwa wategemezi,” amesema Msigwa.