Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKAZI wa Tabata Segerea, jijini Dar es Salaam, Karimu Mwema, amefanikiwa kukabidhiwa fedha zake Sh milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa ya Biko Buku Nibukue iliyofanyika Jumapili.
Akipokea zawadi hiyo leo Alhamisi Februari 3, 2022 katika Tawi la CRDB Premier lililopo Palm Beach jijini Dar es Salaam, Mwema amesema kwanza atapata ushauri wa kifedha kuhusu fedha hizo ili kuweza kukamilisha malengo yake.
“Kwanza kabisa baada ya kupata elimu kutoka kwa wataalamu wa masula ya kifedha nitaendeleza kilimo kwani nina mashamba yangu mkoani Morogoro, hivyo jambo la msingi watu wanedelee kucheza biko kwani ni ya kweli, na inasaidia kutimiza ndoto zao,” amesema Mwema.
Makabidhiano hayo yameendeshwa na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kwa kushirikiana na Balozi wake Kajala Masanja, huku upande wa CRDB, ukiwakilishwa na Meneja wa Tawi hilo, Pendo Kitula na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa tawi hilo, Catherine Momburi.
Biko ni mchezo unaochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unachezwa kwa kufanya miamala kuanzia sh 1000 na kuendelea, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba 2456, bila kusahah wanaocheza kwa mtandao www.biko.co.tz.
Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.